November 27, 2020

 


NAHODHA wa Timu ya Taifa ya Tanzania ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes, Kelvin John anakuwa ni Mtanzania wa pili kusepa na mpira baada ya kufunga hat trick yake ya kwanza jana Novemba 26 kwenye ushindi wa mabao 8-1 dhidi ya Somalia.

John alipachika mabao hayo kwenye mchezo wa pili wa Mashindano ya Cecafa ambayo yanafanyika Arusha, Karatu na Tanzania wakiwa ni wenyeji kwenye mashindano hayo ambayo yana ushindani mkubwa.


Wakati Ngorongoro Heroes ikishinda mabao hayo nane John alitupia mabao yake dakika ya 28,33 na 55 huku mengine yakitupiwa na Hamis Seleiman dk 3, Kassim Haruna dk 47, Frank George dk 65 na msumari wa mwisho ulipachikwa na Anuar Jabir dk ya 86.


Lile la kufuta machozi kwa Somalia lilipachikwa na Sahal Muhammad dk ya 6. Hat trick ya kwanza kwa Ngorongoro Heroes ilipatikana kwenye mchezo wa ufunguzi uliochezwa Novemba 22  na mtupiaji alikuwa ni Abdul Hamis ambaye alifunga mabao yake dk ya 65,71 na 90 wakati Ngorongoro Heroes ikishinda mabao 6-1.


Mechi zote za Ngorongoro Heroes zilichezwa Uwanja wa Black Rhino Academy na imetinga hatua ya nusu fainali ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Jamhuri Kihwelo, 'Julio'.


Kwenye mechi mbili Ngorongoro Heroes imeweka rekodi ya kufunga jumla ya mabao 14 na kufungwa mabao mawili rekodi ambayo ni nzuri ikiwa itakuwa na mwendelezo katika mashindano yote ya ushindani.


Akizungumza na Saleh Jembe, Julio ameweka wazi kuwa ushindani ni mkubwa na vijana wanapambana ili kupata matokeo chanya kwenye mechi zote.

1 COMMENTS:

  1. Somalia,Djibouti hao hata Arusha combine wanawafunga wasibweteke hajacheza mechi ngumu bado.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic