November 2, 2020


 BAADA ya jana, Novemba Mosi kufunga bao lake la nne nyota mzawa, Yusuph Mhilu anaingia anga za Meddie Kagere mshambuliaji namba moja wa Simba.


Mhilu alipachika bao hilo dakika ya 69 wakati timu yake ya Kagera Sugar ikisepa na pointi tatu za Mtibwa Sugar Uwanja wa Kaitaba.


Bao la kwanza kwa Mtibwa Sugar lilipachikwa na Vitalis Mayanga ingizo jipya ndani ya timu hiyo akitokea Klabu ya Ndanda likiwa ni bao lake la kwanza kwa msimu wa 2020/21.  

Lile la Mtibwa Sugar lilipachikwa na Awadh Juma dakika ya 43 naye pia amefunga bao lake la kwanza ndani ya ligi.


Kibarua kingine kwa Kagera Sugar ni Novemba 4 ambapo watashuka uwanjani kusaka pointi tatu mbele ya Simba inayonolewa na Sven Vandenbroeck.


Timu zote zinakutana zikiwa zimetoka kusepa na pointi tatu uwanjani ambapo Simba wao walitoka kumalizana na Mwadui FC kwa kuinyoosha mabao 5-0.


Mhilu anaingia anga za Kagere ambaye naye ametupia mabao manne, mzawa mwingine mwenye mabao manne ni Adam Adam anayekipiga ndani ya JKT Tanzania inayonolewa na mzawa, Abdalah Mohamed,'Bares'.


2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic