KOCHA mkuu wa Biashara United ya Mara Francis Baraza amesema sababu kuu iliyopelekea timu ishindwe kupata matokeo katika mchezo wao dhidi ya Yanga ni wachezaji wake kushindwa kujiamini.
Oktoba 31, Biashara United ilikubali kichapo cha bao 1-0 mbele ya Yanga kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Karume, Mara.
Baraza amesema :“Wachezaji wangu kwenye mchezo wetu na Yanga walishindwa kujiamini na kusababisha kufanya kosa moja ambalo limezaa bao na hiyo imetokana na jinsi Yanga walivyokuwa wanatumia nguvu kutaka kupata ushindi.
"Kwa namna mambo yalivyo naamini kwa
michezo mingine ijayo tutapambana kuhakikisha timu yangu inapata matokeo.”
“Mipango ya mchezo wetu na Yanga
ilinipelekea wachezaji wangu wengi kuwabadilisha nafasi kutokana na mchezo
wenyewe kuwa mgumu kitendo hicho niliona kama kilinisaidia sana maana niliona
wachezaji wangu wakijituma sana lakini mwisho wa siku matokeo hayakuwa upande
wetu lakini tutajipanga kuhakikisha timu inapata matokeo katika michezo ijayo.
"Kiujumla nimeridhishwa na jinsi
timu yangu ilivyocheza kwakuwa ukicheza na timu kama Yanga kisha ukachezesha
wachezaji tena kwa kuwabadilishia nafasi wanazocheza na unafungwa bao 1-0,
kiukweli nawapongeza wachezaji wangu na kwa sasa makosa ni madogo sana ambayo
tutayafanyia kazi ili tuweze kuwa fiti zaidi”
Mchezo ujao kwa Biashara United kwenye ligi ni dhidi ya KMC ambayo imetoka kushinda mabao 3-0 dhidi ya Gwambina FC, Uwanja wa Gwambina Complex.
0 COMMENTS:
Post a Comment