November 19, 2020


 INAELEZWA kuwa mshambuliaji wa Simba Charles Ilanfya na kiungo mkata umeme Gerson Fraga hawapo kwenye mipango ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck kutokana na sababu mbalimbali.


Ilanfya yeye ni mshambuliaji mzawa maisha yake ndani ya Simba yamekuwa na stori ndefu baada ya kuibukia huko akitokea Klabu ya KMC.


Simba ikiwa imecheza mechi 10 yeye ameanza kwenye mechi moja ilikuwa dhidi ya Tanzania Prisons wakati Simba ikifungwa bao 1-0 Uwanja wa Nelson Mandela na alitolewa kabla ya dakika 90 nafasi yake ikachukuliwa na Miraj Athuman.


Pia alipata nafasi kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Azam Complex dhidi ya African Sports alishindwa kuonyesha makeke jambo ambalo limemfanya Sven kumuweka kando kwenye mipango kazi yake.


Nyota mwingine ambaye anampasua kichwa kwa sasa Sven ni Fraga maarufu kama mkata umeme ambaye huyu anasumbuliwa na majeraha ya goti aliyopata kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Biashara United wakati Simba ikishinda mabao 4-0.


Kuumia kwa Fraga kumemfanya Sven aweke wazi kuwa hatamtumia kwenye mechi zake zote zilizobaki kutokana na kuwa nje kwa muda mrefu akitibu majeraha yake.


Kuhusu Fraga, Sven amesema:"Sitakuwa na Fraga kwenye mechi zangu zijazo ikiwa ni pamoja na ile ya Ligi ya Mabingwa Afrika hivyo anahitajika kutafutwa mbadala wake haraka,".

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic