November 29, 2020


 BONDIA Iddi Pialali wa Bagamoyo Pwani hapa nchini, leo alfajili amefanikiwa kumtwanga Bondia wa Kimataifa Arnel Tinampay kutoka Ufilipino.

Tinampay alikubali kichapo hicho kwenye pambano la raundi nane lililopigwa Ukumbi wa Next Door Arena uliopo Masaki Jijini Dar.


Katika pambao hilo mabondia wote walianza kushambuliana kwa kasi kila mmoja akionekana kutaka kumlaza mwenzake kwa KO lakini kutokana na umahiri waliouonesha walijikuta wote wakimaliza raundi zote nane.


Wawili hao baada ya kumaliza pointi hizo majaji wa mpambano huo walimpa ushindi Pialali kufuatia kumtwanga ngumi Mfilipino huyo na kutaka kumuangusha mara kadhaa hali iliyopelekea aonekane kujikongoja ilimradi amalize pambano hilo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic