November 17, 2020


 KIUNGO wa kati wa Manchester United na Ufaransa, Paul Pogba, anasema kwa sasa anapitia kipindi kigumu sana cha kazi yake ya soka kutokana na muda wake wa mchezo katika Old Trafford.


Nyota huyo kwa sasa hana uhakika wa kuanza kikosi cha kwanza chini ya Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solksjaer jambo linalomfanya afikirie kusepa ndani ya kikosi hicho.


Habari zinaeleza kuwa mabosi wa United kwa sasa wapo tayari kumuuza nyota huyo anayecheza timu ya Taifa ya Ufaransa.

Akifanyiwa mahojiano na kituo cha RTL Pogba  amesema kuwa; “Napitia kwenye wakati mgumu sana kuliko wakati wowote ule katika maisha yangu ya soka.  Timu ya taifa ndiyo imekuwa kama pumzi ya mimi kuja kupumulia huku, ni mahali safi, nafurahia zaidi,".

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic