November 17, 2020


 MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba, Mohamed Dewji (Mo) amefunguka kuwa, katika vipaumbele ambavyo wametaka kuvifanyia kazi ni pamoja na kuboresha maslahi ya timu ya Simba Queens pamoja na benchi la ufundi.


Mo alisema licha ya kuwa timu hiyo ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake msimu uliopita imekuwa haipati kile inachostahili kutokana na wachezaji wa timu hiyo kutokuwa na mikataba rasmi ya kufanya kazi ndani ya klabu hiyo.

Mo aliyasema hayo wikiendi iliyopita alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari za michezo kwenye ukumbi wa mikutano uliopo kwenye ofisi yake Posta jijini Dar es Salaam ambapo aliweka wazi kuwa wao kama viongozi wana mipango endelevu na ya muda mrefu kwa timu hiyo.

"Tunahitaji kuboresha maisha, maslahi ya Simba Queens kwa maana ya wachezaji na benchi la ufundi. Unajua hawa wachezaji licha ya msimu uliopita kuwa mabingwa walikuwa hawapati wanachostahili kutokana na ukweli kwamba wengi hawana mikataba rasmi.

"Kwahiyo tumeanza kwanza na wachezaji ambao watakuwa wanahitajika na benchi la ufundi kwa ajili ya msimu ujao. Hii timu tuna mipango nayo ya muda mrefu na tunaipenda sana," amesema Mo.

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic