November 7, 2020


KUELEKEA mchezo wa watani wa jadi, Yanga dhidi ya Simba, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa, ametoa onyo kali kwa wale watakaothubutu kung’oa viti na kufanya vurugu kwenye mchezo huo.

Msimu wa 2016/17, timu hizo zilicheza ambapo zilitoka sare ya bao 1-1, bao la Yanga lilifungwa na Amisi Tambwe ambapo mashabiki wa Simba walifanya vurugu na kung’oa viti.

Yanga inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar, leo Jumamosi.

Msimu wa 2016/17, timu hizo zilipocheza zilitoka sare ya bao 1-1 lakini bao lililofungwa na Amisi Tambwe, lilisababisha mashabiki waliodhaniwa kuwa ni wa Simba (kutokana na rangi ya nguo zao na upande waliokuwa wamekaa) kung'oa viti.

Akizungumza jijini Dar, Kamanda Mambosasa alisema kuwa kwenye mpira wa miguu kuna matokeo matatu hivyo mashabiki wakubaliane na lolote litakalotokea.

“Mpira una matokeo matatu kuna ushindi, kushindwa na kutoa sare na wajiepushe na mihemko ya kishabiki, mara nyingi baada ya kushindwa watu wanahangaika kung’oa viti kwani viti vinakosa gani, leo umeshindwa na kesho utashinda, suala la kuharibu mali na kufanya vurugu ni uchwara kwenye ushabiki, niwaombe wawe watulivu, wanadi timu zao na wajiandae kwa matokeo,” alisema kamanda huyo. 

6 COMMENTS:

  1. Usimumunye maneno wala usipepese macho ndugu mwandishi sema MIKIA WALING'OA VITI kwa Mkapa!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Na marefa wenu wakizingua tunang'oa tena mbona hajazungumzia wale wanaovamia washabiki wa timu nyingine

      Delete
  2. Kipindi mile mlizowea sana kutusumbua na malinzi wenu ndomaana bado ananyea debe huko mnafunga magori ya mikono anawachekea tu safari sisi tunatoa vipigo tu mpaka mseme simba baba lao

    ReplyDelete
  3. Thubutu tena kung'oa kitu uone, enzi hizi za magufuri hata uende wapi lazima tukunase tu fanya tena upuuzi wenu nyie nguruwe fc.

    ReplyDelete
  4. Mwandishi acha ushamba, zimechezwa mechi ngapi na viti havijang'olewa.... Mbona huongelei kupiga refa na kushambulia magari ya timu pinzani kwa mawe

    ReplyDelete
  5. Marefa ndo chanzo Cha vitu kung'olewa, wakichezesha fair hakuna atakayeng'oa kiti. Ila utopolo waache uhuni wakuwavamia wenzao Kama hawawezi ushabiki wakalale tu au wakatazame kwenye vibandaumiza. Kesho utopolo anachapwa bakora so chini ya tano na ikiwezekana itaweka record kwakuchwapwa bakora nyingi msimu huu, angalizo wasimfukuze kocha.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic