November 15, 2020

 




FRANCIS Baraza, Kocha Mkuu wa Biashara United amesema kuwa malengo makubwa ya timu yake ni kumaliza ndani ya tano bora kwa msimu wa 2020/21 ndani ya Ligi Kuu Bara.

Biashara United ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 17 baada ya kucheza mechi 10 kwa msimu huu.

Akizungumza na Saleh Jembe, Baraza amesema kuwa mipango ipo sawa na kwa sasa wanaendelea kujiweka sawa kwa ajili ya mechi zao zijazo.

"Kikosi kipo vizuri na wachezaji wapo tayari kwa ajili ya ushindani wa mechi zetu zote ndani ya ligi.

"Kila mmoja anatambua kwamba ligi ina ushindani nasi pia tunashindana kufanya vizuri zaidi kwenye mechi zetu kwa kuwa malengo yetu ni kumaliza ndani ya tano bora.

"Hilo linawezekana, mashabiki waendelee kutupa sapoti hatutawaangusha," amesema.

Ikiwa imefunga mabao sita, mtupiaji wao namba moja ni Kelvin Friday mwenye mabao mawili na moja ya pasi  ya bao lake la kwanza ndani ya ligi alipewa na Gerald Mdamu.

1 COMMENTS:

  1. Mbona kichwa cha habari hakikubaliani kabisa na maelezo?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic