November 17, 2020

 


INAELEZWA kuwa Simba inavutiwa na kiungo wa  Kaizer Chiefs na timu ya Taifa ya  Kenya Anthony Teddy Akumu.


Hesabu za Simba ni kuinasa saini yake ili aje kuziba nafasi ya kiungo wao alieumia raia wa Brazil Gerson Fraga ambaye amewekwa kando na Kocha Mkuu Sven Vandenbroeck.

Fraga ambaye alikuwa ni chaguo la kwanza la Sven kwenye mechi zake za hivi karibuni majeraha yake ni ya muda mrefu jambo ambalo litawafanya Simba wakose huduma yake.

Alipata majeraha ya goti wakati timu yake ikipambana mbele ya Biashara United Uwanja wa Mkapa na ilishinda mabao 4-0.

Habari zimeeleza kuwa tayari mpango wa kuachana na Fraga umekamilika kwa kuwa Sven mwenyewe ameshatoa ripoti kwa mabosi kwamba hatamtumia kwa muda mrefu jambo ambalo limewapa nguvu ya kusaka mchezaji mwingine atakayeziba pengo lake na jina la kiungo huyo wa Kenya likitajwa.


Kupitia kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Mohamed Dewji, 'Mo' amesema kuwa watafanya usajili kulingana na ripoti ya kocha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic