JUMA Mwambusi, kocha msaidizi wa Yanga amesema kuwa uwezo walionao wachezaji wao unawapa nafasi ya kupata matokeo chanya kwenye mechi zao watakazocheza.
Kwenye Ligi Kuu Bara Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 24 baada ya kucheza mechi 10.
Haijapoteza mchezo mpaka sasa ikiwa imefungwa mabao matatu pekee na kufunga mabao 12.
Mchezo wake unaofuata ni dhidi ya Namungo FC, Novemba 22, Uwanja wa Mkapa saa 1:00 usiku.
Mwambusi amesema:"Wachezaji wanatambua majukumu yao na kila mmoja yupo tayari kwa ajili ya kuona timu inapata matokeo chanya hivyo kazi bado ipo na tutaendelea kupambana.
"Kikubwa ambacho kipo ni kwamba timu inahitaji kurejea kwenye ubora wake na hesabu kubwa zipo kwenye kutwaa ubingwa ili hayo yatimie ni lazima kila mmoja acheze kwa juhudi na kutimiza malengo," .
0 COMMENTS:
Post a Comment