November 26, 2020


 UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa wamepokelewa vizuri nchini Nigeria baada ya kuweka maandalizi ya awali na timu hiyo itakuwa kwenye ulinzi chini ya Serikali ili kuimarisha usalama kutokana na hali ya nchini Nigeria kutokuwa salama muda wote.


Kikosi hicho kiliwasili salama Nigeria jana, Novemba 25 ambapo mratibu wa Simba, Abas Ally alitangulia mapema kuweka mipango sawa.


Mratibu huyo amesema kuwa mazingira ya Nigeria ni mazuri na alipata ushirikiano mkubwa kutoka chama cha soka cha nchini Nigeria.


Aliongeza kuwa usalama wa hali ya Jos inaeleweka kuwa haipo sawa kwa wageni ambao wanafika ila kwa wenyeji wao wanaona kila kitu kinakwenda sawa lakini Simba imeweka wazi kwamba kwa mujibu wa wenyeji wao wamewaambia kwamba watawapa sapoti na kuwapa ulinzi wachezaji pamoja na benchi la ufundi.


Taarifa kutoka Simba zimeeleza kuwa kikosi leo kitaanza rasmi mazoezi Abuja, Nigeria kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Plateau FC ambao utapigwa siku ya jumapili, Novemba 29, 2020 kwenye uwanja wa New Jos uliopo mji wa Jos kuanzia saa 10:00 jioni (saa 12:00 jioni - Tanzania).

4 COMMENTS:

  1. Wawe makini sana, adui hawezi kukuwekea ulinzi halisia ila wa kimizengwe

    ReplyDelete
  2. Inawezekana maana Kuna wale mashabiki wa timu pinzani ambao hawaitakii hiyo timu mema kama tulivyo sisi kwa yanga

    ReplyDelete
  3. Mara zote Simba ilipoenda kucheza na Enyimba haikuwahi kufanyiwa hujuma. Kuna nchi zinajitambua kwa soka.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic