TIMU ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake chini ya miaka 17 leo Novemba 8 imeibuka na ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya timu ya Taifa ya Wanawake ya Afrika Kusini kwenye mchezo wa mashindano ya Cosafa.
Huu ni mchezo wa tatu wa Tanzania ambapo mchezo wa kwanza ilishinda mabao 5-1 dhidi ya Comoro kisha ikachapwa mabao 2-1 dhidi ya Zimbabwe na leo imeibuka na ushindi huo mbele ya Afrika Kusini.
Shukrani kwa Aisha Masaka wa Tanzania ambaye ameibuka kuwa nyota wa mchezo baada ya kufunga mabao matano kwenye mchezo mmoja huku akisepa na mpira wake jumlajumla.
Alipachika mabao hayo dakika ya 21,23,39,44 na 89 na lile moja la mwanzo kabisa lilifungwa na Mwamvua Haruna dakika ya 18.
Bao pekee la kufuta machozi kwa Afrika Kusini lilifungwa na Noela Luhala ambaye alijifunga dakika ya 79 Uwanja wa Oval.
Hawa madada wetu ni noma sana.
ReplyDelete