November 9, 2020


 MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu England Liverpool wanazidi kuingia kwenye majanga baada ya jana Novemba 8 beki wao Trent Alexander Arnold kupata majeraha ya misuli wakati timu hiyo ikilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Manchester City Uwanja wa Etihad.


Beki huyo alifanyiwa mabadiliko dakika ya 63 baada ya kushuhudia bao la kwanza kwa timu yake likifungwa na Mohamed Salah dakika ya 13 kwa penalti na lile la City dakika ya 31 na Gabriel Jesus atakosekana kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya England ambayo itakuwa na mchezo dhidi ya timu ya Taifa ya Ireland Novemba 12 na  Novemba 15  dhidi ya timu ya Taifa ya Ubelgiji kwenye mashindano ya Nations League.

Klopp amesema kuwa Trent atakuwa nje ya kikosi cha timu ya Taifa ya England kutokana na hali aliyonayo mpaka pale atakapokuwa fiti kwa kuwa hakuna anayetambua hali yake mpaka pale atakapofanyiwa vipimo.

Hii ni taarifa mbaya kwa mashabiki wa Liverpool hasa kwa upanda wa beki kwa kuwa tayari Klopp anapambania taji la Ligi Kuu England bila ya uwepo wa beki wake kisiki wa kati Virgil Van Dijk ambaye atakuwa nje ya uwanja msimu mzima na nyota wake mwingine Fabinho anatarajiwa kurejea uwanjani baada ya mapumziko ya timu ya Taifa kuisha.

Klopp amesema:"Trent anaweza kuwa nje kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya England, bado hatujajua kwamba anaweza kuwa bora lini mpaka pale ambapo tutamfanyia vipimo.

Nyota mwingine ambaye anaweza kukosa kutumika ndani ya timu ya Taifa ya England ni mshambuliaji wa Manchester United,  Marcus Rashford ambaye huyu anasubiri ripoti za madakatari wa timu ya taifa kwamba kama anaweza kuwa sehemu ya kikosi ama la.

Ole Gunnar Solskjaer, Kocha Mkuu wa Manchester United amesema kuwa nyota huyo alipata maumivu kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Everton wakati Manchester United ikishinda mabao 3-1 Uwanja wa Goodison Park.

"Ana maumivu ya bega na wakati ninamfanyia mabadiliko alionekana hayupo sawa anakuwa ni mchezaji wa tatu kupata majeraha kwenye Uwanja wa Goodison Park," amesema Solskajer.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic