November 9, 2020


 KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa walistahili kupewa penalti kwenye Dar Dabi iliyochezwa Novemba 7 Uwanja wa Mkapa na timu zote kuambulia pointi mojamoja baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1.


Yanga ambao walikuwa wenyeji wa mchezo huo walianza kupata bao la kuongoza dakika ya 31 kupitia kwa Michael Sarpong kwa mkwaju wa penalti uliompoteza mlinda mlango namba moja wa Simba Aishi Manula na lile la Simba lilifungwa na Joash Onyango.


Onyango ambaye ni beki kisiki ndani ya Simba alifunga bao hilo dakika ya 86 na kumfanya afute makosa aliyoyafanya dakika ya 28 na kufanya Yanga wapewe penalti kwa kuwa mwamuzi wa kati Abdalah Mwinyimkuu alitafsri kwamba alimchezea faulo Tuisila Kisinda.


Sven amesema kuwa:"Kwenye mchezo wetu dhidi ya Yanga nafikiri tulipaswa kupewa penalti kwa kuwa wachezaji wangu walichezewa madhambi mengi na wapinzani wetu.


"Lakini kwa kuwa ni mpira na maamuzi yameshatolewa basi ni wakati wetu wa kufanya maandalizi kwa ajili ya wakati ujao ili kuzidi kuwa bora.


"Ligi ina ushindani na kila mmoja anahitaji ushindi hivyo mashabiki wazidi kutupa sapoti kwani kazi ipo na tutazidi kupambana ili kuwa bora," amesema.


Simba kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 20 baada ya kucheza mechi 10 ndani ya ligi kwa msimu wa 2020/21.

Vinara ni Azam FC wenye pointi 25 huku nafasi ya pili ipo mikononi mwa Yanga yenye pointi 24 zote zimecheza mechi 10.

5 COMMENTS:

  1. Miaka zaidi ya 3 Yanga inalalamikia Marefa na ninyi mikia mlikuwa mnawabeza na kusema wamezidi kulalamika. Sasa ninyi hili moja tu mnavunja rekodi ya kulalamika. Hakuna asiyejua udhaifu wa marefa wetu na wanafanya hayo ni kudhihirisha kuwa uwezo wao wa kutafsiri sheria ni mdogo. Msilalamike kuwa Yanga inabebwa wakati nayo inalalamika mara nyingi tu. Ninyi mmesema Yanga inabebwa kwa kuangalia mechi ya Jana tu. Mbona wakat Yanga inalalamika ninyi mnasema Yanga wanalalamika mambo ya uongo. Kuweni weledi basi kukemea udhaifu wa marefa ili tuinue kiwango cha soka Tanzania. Hiyo TFF ambavyo imejaa Simba tupu wanawezaje kuweka marefa wenye mikakati ya Kuipendelea Yanga wakati wao wooooootee mpaka wafagiaji ni Wanasimba

    ReplyDelete
  2. Kocha anawafanya viongozi wa Simba wapoteze focus juu ya kuporomoka kwa kiwango cha timu yake, amefungwa mechi 2 mfululizo na amenusurika kufungwa na Yanga, ashukuru kutoka kwa Lamine Moro, kukosa goli la wazi kwa Farid Musa, kutolewa kwa Sarpong na Farid kulikopelekea Yanga kubaki kujilinda zaidi hatimae shomari kapombe akapanda na kutoa krosi iliyosababisha kona, hapo kabla ilikuwa vigumu kupanda kwa mabeki wa pembeni wa simba kwakuwa sarpong na farid walikuwa kila mara wanaelekea golini kwao. Sven moyoni anashukuru kwa sare hii, kwani kama angefungwa angefukuzwa na kupoteza kibarua chake, alivyo mjanja kucheza na fikra finyu za waafrika anageuka kama mshabiki na mpenzi maandazi kulalamikia maamuzi ya refarii, aendelee kuwapumbaza tu ili ukweli ni kuwa kiwango cha simba kimeshuka na pengine hana jipya tena na wachezaji hawana mbinu mpya kwani sio Yanga tu hata Ruvu shooting na Tz prison wanajua kuithibiti falsafa ya Sven, bado Simba itafungwa sana kwa mechi zijazo na timu nyingine labda viongozi wawasaidie kununua mechi kabla ya mchezo ili uwanjani muende kutimiza wajibu tu. Sven timu imekushinda ni wakati wako kuondoka kabla mambo hayajaharibika zaidi.

    ReplyDelete
  3. Kukosa magoli ya 'wazi' kwy mpira ni jambo la kawaida. Hata simba pia mechi ya Jmosi alikosa magoli, kama alivyokosa Boko na Kapombe.

    ReplyDelete
  4. Tatizo la kujifunzia mpira ukubwani eti kiwango cha Simba kimeshuka wamefungwa mechi mbili, mwaka jana simba kachukua ubingwa kafungwa mechi nne. Kocha wenu anashukuru kutoa sare na simba nyinyi huku washabiki ndo mnajifanya mnapiga kelele yani utopolo akili zenu wengi ni hamnazo

    ReplyDelete
  5. Tuache ushabiki wa hovyo kama mechi ya juzi iliokuwa na maamuzi ya upande mmoja kwa upendeleo kwa Yanga ingekuwa ndio simba aliebebwa basi hivi sasa ungesikia kila aina ya matusi na kejeli kutoka wakilalamikia simba kubebwa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic