November 10, 2020

 


SHEHAT Mohame ameibuka kuwa mchezaji bora leo Novemba 10 wakati timu ya Taifa ya Wanawake U 17 ikishinda mabao 10-1 dhidi ya Zimbabwe kwenye mashindano ya Cosafa nchini Afrika Kusini.

Mohame alitupia mabao mawili dakika ya 18 na 89 huku mengine yakifungwa na Protasia Kipaga dakika ya 1,Koku Kipanga dakika ya 11, Irene Kisisa dakika 13, Ester Mabaza dakika ya 32.


Zawadi Athuman dakika ya 55, Asha Masaka naye alitupia mawili dakika ya 71 na 82, Rudo Machadu alitupia dakika ya 79 kwa upande wa Zimbabwe na kufanya liwe bao lao pekee la kufutia machozi.


Ushindi huo mnanono unaifanya U 17 kutinga hatua ya fainali ya mashidano ya Cosafa yanayofanyika nchini Afrika Kusini na inafikisha jumla ya pointi 9.


Fainali itakuwa ni dhidi ya Zambia kwenye mchezo unaotarajiwa kuchezwa Novemba 11 Uwanja wa Oval. 


5 COMMENTS:

  1. TFF iwekeze kwenye soka la wanawake kwa nguvu sawa na wanavyofanya kwa wanaume. Soka la wanawake linaipatia sifa Tanzania zaidi ya soka la vwanaume

    ReplyDelete
  2. Kweli kabisa penye juhudi panahitaji support wametoa kipigo cha mbwa mwizi.Hongereni sana madogo.

    ReplyDelete
  3. Wana wake bwana ndo mna funga mabao meng hvyo kwel et 10 ya moja du hongelen

    ReplyDelete
  4. Hongereni sana. Viongozi wetu tunaomba na tunashauri vijana hao waendelee kutunzwa na kusimamiwa ili waweendelevu Tanzania.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic