November 22, 2020


 LEO Liverpool ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Leicester City kwenye mchezo wa Ligi Kuu England Uwanja wa Anfield majira ya saa 1:15.


Ni raundi ya tisa ambapo Liverpool ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya wapinzani wake ambao wana pointi 18 kibindoni huku wao wakiwa na pointi 17.

Mabingwa watetezi msimu uliopita waliweza kutwaa taji la Ligi Kuu England bila kupoteza kwenye Uwanja wa Anfield hivyo leo wana kazi ya kuendelea kulinda rekodi hiyo licha ya kuwakosa nyota wake muhimu ikiwa ni pamoja na mshambuliaji wao Mohamed Salah abaye ameripotiwa kuwa na Virusi vya Corona.

Leicester City ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Brendan Rodgers imeanza msimu vizuri licha ya kutokuwa na matokeo mazuri mbele ya Liverpool kuna jambo leo linaweza kutokea kwa kuwa waliweza kuitungua Manchester City mabao 5-2 ikiwa Uwanja wa Etihad.

Ukuta wa Liverpool umeyumba kidogo kutokana na lundo la majeruhi ikiwa ni pamoja na beki kisiki, Virgil van Dijk, Joe Gomez, Trent Alexander huku Andy Robertson akiwa na hatihati ya kuukosa mchezo wa leo kwa kuwa naye aliumia kwenye timu ya taifa. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic