November 22, 2020

 


SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa sababu kubwa iliyofanya kiungo wake namba moja ndani ya Simba, Jonas Mkude kukosa mchezo wa jana Novemba 21 dhidi ya Coastal Union ni kuchelewa kuripoti kambini.


Jana Coastal Union ilikubali kufungwa mabao 7-0 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid na Simba huku Mkude akiwa ni miongoni mwa wachezaji waliokosa mchezo huo. 


Wengine wa Simba ambao walikosa mchezo huo ni pamoja na Luis Miquissone na Meddie Kagere waliochelewa kuripoti kambini kutokana na kuwa kwenye timu zao za Taifa na Chris Mugalu na Gerson Fraga ambao ni majeruhi.


Sven amesema:" Mkude alichelewa kurudi kambini baada ya kutoka kwenye timu ya taifa wakati wenzake wakiwa wamerejea kwa wakati sahihi.


"Kwa hiyo mechi dhidi ya Coastal Union alikuwa na adhabu ya kinidhamu ya kuukosa mchezo huo kutokana na suala hilo la nidhamu ambalo amelifanya,".

Simba imefikisha jumla ya pointi 23 ikiwa nafasi ya tatu na vinara wa ligi ni Azam FC wenye pointi 25 huku wakifuatiwa na Yanga iliyo nafasi ya pili na pointi 24.

5 COMMENTS:

  1. Mmmhhh wachezaji wa kitanzania bwana ni shida kweli kweli

    ReplyDelete
  2. Hawa ndyo wachezaji wa bongo, wenzie akina Boko, Manula, Nyoni, Ndemla, Kapombe, Tshabalala, Dilunga wote walikuwa Taifa stars na waliwahi kurudi, yeye alikuwa timu ya taifa gani?

    ReplyDelete
  3. Hawa ndyo wachezaji wa bongo, wenzie akina Boko, Manula, Nyoni, Ndemla, Kapombe, Tshabalala, Dilunga wote walikuwa Taifa stars na waliwahi kurudi, yeye alikuwa timu ya taifa gani?

    ReplyDelete
  4. Huyu pimbi kuna mtu anampa kiburi lakini yana mwisho na mwisho wenyewe huko mbali

    ReplyDelete
    Replies
    1. MWISHO WAKE UNAKUJA, SI ULIONA ALICHOKIPATA JUUKO MURSHID? TEDY AKUMU, KOTEI NA TSHISHIMBI WAMO KWENYE LIST YA KIUNGO MKABAJI YA DIRISHA DOGO LA DECEMBER 15, NYONI JANA KAONYESHA UBORA WAKE, AMECHEZA SOKA SAFI SANA KULIKO KAWAIDA

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic