UWANJA wa Mkapa
FT: Yanga 1:1 Namungo
Mpira umekamilika Uwanja wa Mkapa kwa timu zote kugawana pointi mojamoja baada ya dakika 90 kukamilika.
Metacha Mnata kipa wa Yanga amekuwa ni shujaa baada ya kuokoa penaltii iliyopigwa na mshambuliaji namba moja wa Namungo mwenye mabao manne, Bigirimana Blaise dakika ya 90.
Novemba 22, mchezo wa Ligi Kuu Bara
Kipindi cha pili
Dakika ya 90+2 Blaise anapiga penalti inaokolewa na Mnata
Dakika ya 90 Mwamnyeto analewa kadi ya njano
Dakika ya 80 Carlos Carinhos anapaisha faulo
Dakika ya 69 Shamte anaingia anatoka Miza law Namungo
Dakika ya 68 Sarpong anapewa huduma ya kwanza
Dakika ya 67 Mabeki wa Namungo wanatibua mipango
Dakika ya 57 Carinhos anapiga shuti linaokolewa na Nahimana
Dakika ya 55 Farid Mussa anatoka anaingia Deus Kaseke
Dakika ya 54 Nahimana anaokoa
Dakika ya 53 Carinhos anachezewa faulo na Sey anaonyeshwa kadi ya njano
Dakika ya 51 Mnata anaokoa hatari
Dakika ya 46 Hamis Mgunya anaonyeshwa kadi ya njano
Kipindi cha kwanza:-Yanga 1-1
Namungo
Mapumziko Uwanja wa Mkapa
Zinaongezwa dakika 2
Dakika 45 zinakamilika
Dakika ya 44 Carlos Carinhos anapiga nje ya lango
Dakika ya 43 Blaise anapoteza pasi
Dakika ya 41 Sey anapaisha nje kidogo ya 18
Dakika ya 40 Sarpong anachezewa faulo
Dakika ya 37 Carlos Carinhos anapewa huduma ya kwanza
Dakika ya 33 Fei Toto anamchezea faulo Lukas Kikoti anapiga shuti linakwenda nje ya lango
Dakika ya 30 Yanga wanaanzisha faulo baada ya Lamine Moro kuchezewa na nyota wa Namungo
Dakika ya 28 Namungo wanaanzisha faulo
Dakika ya 22 Tuisila anafanya jaribio ndani ya 18 halileti matunda
Dakika ya 21, Metacha Mnata anaokoa shuti la Bigirimama Blaise
Dakika ya 16 Goaaal Namungo kupitia kwa Stephen Sey
Dakika ya 15 Edward Manyama anapiga mpira wa adhabu haizai matunda
Dakika ya 13, Goooooal Yanga kupitia kwa Carlos Carinhos kwa kichwa.
Dakika ya 9 mwamuzi anasema Bigirimama ameotea
Dakika ya 6 Carlos Carlinhos anapiga kona ya pili
Dakika ya 5 Michezo Sarpong anapiga off target ya kwanza
Dakika ya 3 Metacha anaanzisha mashambulizi
Dakika ya 2 Farid Mussa anapiga kona ya Kwanza kwa Yanga
Wapigwe vyura hao
ReplyDeleteutopolo wakitoka salama wakatambike
ReplyDeleteTutatoka kifua mbele na point tatu huku tukisubiri kicheko wiki ijayo
DeleteEti Saleh Jembe anasema kocha wa Yanga naye ni mpya!Wakati keshafundisha mechi karibu 4 au tano na tuzo ya kocha bora kapata..Ndiyo mpya huyo?
ReplyDeleteMnatoa updates kama hamtaki
ReplyDeletehebu soma kule bado ngapi? na mnazidiwa magoli ya kufungwa 16.Nyie fungeni kamoja wakati wenzenu ni mwendo wa zaidi ya tatu!
ReplyDeletePoint 1 ni kubwa kuliko magoli 100, kwahiyo kwenye soka points ndio mpango mzima
ReplyDeleteAaaah kubali tu Amna mpira. Wowote yanga
DeleteNdugu Kaze jitayarishe kuzomewa
ReplyDeletekaze na kamprotic ni walewale.
DeleteTangu Kaze ametua timu haina tofauti na ya Zlatko..Ki uhalisia Yanga inachofanya ni sawa na Yanga ile ya Zahera..Poleni zana bilioni moja na nusu zimepotea kwenye mtaro wa maji.Leo mmeponea chupuchupu...Na mechi iliyopita aliwaokoa refa...msijali kwani bahati mnayo kila siku
ReplyDeletePointi zinayeyuka. Jumatano watapoteza ointi tena. Azam wamepumzika diku moja extra na hasira za kufungwa. Lazima ajambe mtu.Leo chupuchupu mavi yaguse chupi.
ReplyDeletemechi ya 3 hii sare...je na mechi ijayo ikiwa sare kocha atatimuliwa?
ReplyDeleteYanga mta koma mna jifanya makonk wa game
ReplyDeleteWarundi Ni wabinafsi siku zote ndio maana kaigharimu team
ReplyDelete