UONGOZI wa Yanga umeweka bayana kuwa watani zao wa jadi Simba leo kuwafunga itakuwa ngumu labda waibe matokeo kwa kuwa kikosi kimekamilika kila idara.
Yanga iliyo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 23 inakutana na Simba iliyo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 19 zote zimecheza mechi 9.
Kwa upande wa Yanga ambao ni wenyeji wanajivunia rekodi yao ya kutopeteza mechi ndani ya ligi huku Simba ikiwa imepoteza mechi mbili mfululizo.
Ikumbukwe kuwa msimu wa 2018/19 dabi ya kwanza wakati Yanga ikiwa haijapoteza mchezo zilipokutana Uwanja wa Mkapa, dakika 90 zilikamilika kwa sare ya bila kufungana.
Mechi mbili za msimu uliopita, Yanga waliibuka wababe wa Simba kwa kuifunga jumla ya mabao matatu na kusepa na pointi nne kati ya sita huku Simba ikifunga mabao mawili.
Mchezo wa kwanza Januari 4, Simba 2-2 Yanga na ule wa pili Machi 8, Yanga 1-0 Simba jambo ambalo linaongeza ugumu kwenye mchezo wa leo unaosubiriwa kwa shauku kubwa.
Ofisa Uhamasishaji wa Yanga,Antonio Nugaz amesema kuwa haoni namna ambayo watani zao wanaweza kuepuka kufungwa kwa kuwa kikosi cha Yanga kimekamilika.
“Sioni namna ambayo watani wetu wanaweza kutufunga kwani tuna Bakari Mwamnyeto, Kibwana Shomari, Tuisila Kisinda hawa wote wapo vizuri, sasa labda waibe matokeo ndio itakuwa mbinu yao kupata ushindi,” amesema.
Mna ota nyie vyura
ReplyDeleteNyiemisukule musije na matokeo uwanjani dakika 90 zitaongea
ReplyDeleteAwa wapumbavu wana taka kuja na matokeo uwanjan
ReplyDeleteTAYARI MMEPEWA MATOKEO, AU VIPI UTO?
ReplyDelete