November 19, 2020


 HUENDA mashabiki wa Ligi Kuu England wakaruhusiwa kuingia uwanjani kushuhudia mchezo kati ya Tottenham dhidi ya Arsenal ikiwa tu maambukizi ya Virusi vya Corona yatapungua.


Mashabiki wa England wanatarajiwa kuanza kuruhusiwa kuingia ndani ya uwanja kuanzia Desemba 2020 kushuhudia burudani ambayo walikuwa wameikosa kwa muda mrefu kutokana na dunia kuingia kwenye vita dhidi ya janga la Virusi vya Corona. 

Katika michezo ya Premier ambayo mashabiki wataishuhudia ni pamoja na London Dabi itawakutanisha Tottenham na Arsenal, pia ule dhidi ya Liverpool na Wolves, Chelsea v Leeds, Manchester United v West Ham na mechi zote hizi zinatarajiwa kuchezwa Desemba 5.


Kiongozi wa soka nchini England amepeleka maombi  kwa Serikali ili kuruhusu mashabiki kuanza kuingia uwanjani ifikapo Desemba 2 kwa mujibu wa taarifa ambapo inaelezwa ikiwa mambo yatakuwa sawa kila kitu kitawekwa wazi.


Taarifa zinaeleza kuwa timu ambazo zinatoka kwenye majiji makubwa hazitaruhusiwa kuingiza mashabiki kwa kuwa bado janga hili linaitesa dunia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic