November 12, 2020

 


MENEJA wa kikosi cha Yanga, Hafidhi Saleh, amesema kuwa Yanga haihusiki kwa namna yoyote na makosa ya mwamuzi wa mchezo wa dabi, Abdallah Mwinyimkuu huku akiamini makosa hayo yalifanyika kutokana na upungufu wa kibinadamu.

 

Baada ya mchezo huo ulioisha kwa sare ya bao 1-1, viongozi na mashabiki mbalimbali wa Simba wamekuwa wakitupa tuhuma kali kwa Mwinyimkuu kwa kushindwa kutafsiri kwa ufasaha Sheria 17 za mchezo huo, huku akiishia kuamuru penalti iliyowapa faida Yanga, licha ya tukio hilo kuonekana kuwa na utata.

 

Saleh amesema: “Simba mara zote wamezoea kulalamika, nadhani kuna daraja wamejiweka wanaamini wao sio timu ya kufungwa au hata kutoa sare na ndiyo maana utawaona sio tu kwenye mchezo wa Jumamosi, Simba walilalamika walipofungwa dhidi ya Tanzania Prisons na hata Ruvu Shooting.

 

“Kwangu mimi sioni kama kulikuwa na tatizo lolote kwa mwamuzi zaidi ya ukweli kuwa kuna wakati mwamuzi kama binadamu anaweza kufanya makosa ya kibinadamu na ndicho ambacho kilitokea, hivyo sidhani kama kulikuwa na ulazima wa kumlalamikia mwamuzi au wachezaji.

 


“Kwa kweli nimeshangazwa kuona kiongozi mmoja mkubwa tu wa kikosi hicho akiwashutumu baadhi ya wachezaji wao akiwemo Chama, (Clatous) kuwa walicheza chini ya kiwango eti kwa kuwa wanahusishwa kujiunga na Yanga, hili sio jambo sahihi.”


Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 24, Simba ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 20 zote zimecheza mechi 10.


Chanzo: Championi

16 COMMENTS:

  1. Kwa tunyamaze tuu wakati tunaonewa? Huu sasa upuuzi

    ReplyDelete
  2. Zungumzia na mechi ya kmc mliyopewa penati ya utata na mechi ya gwambina ambayo goli halali lilikayaliwa janja yenu ya kuhonga marefa imejulikana

    ReplyDelete
  3. Baada ya yote hayo kwani mmefanikiwa kuifunga Simba na kweli hilo goli mlilogaiwa kweli mna furaha nalo?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mikia kumbukeni mmeshapigwa mechi 2..na bado

      Delete
  4. Ninyi Simba hamna pesa za kuhonga marefa mpaka mkafungwa mechi 2 mfululizo? Hoja zenu hata mashiko hamna. Kama mlizoea vibudu, vya kuchinjwa hamtoviweza kamwe

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndo mshatwaa ubingwa tyr, upumbavu wa utopolo kutoa sare na Simba kwao ndo tyr washabeba kombe. Wanaume tunarudi mechi bdo nyingi tutakygonga mzunguko wapili zaidi ya mwaka 1977. Ubingwa upo kwetu na utabaki kwetu wanaohujumu mmoja mmoja atawajibishwa senzo wakwanza

      Delete
  5. SIMBA msimu huu mtalalamika sana maana kila refa ameshawaona kuwa ni malalamishi fc, sasa jiandaeni kuumia kunguni nyie

    ReplyDelete
  6. Kwani siku ile tunatoa sare ya 2-2 Kagere alipewa penalty mbona hamkulalamika? Mpira umewashinda wanabaki kukimbilia Police

    ReplyDelete
  7. Nabado mikia wa mo mtalalamikasana mwakahuu zamuyenu mututesana yanga hatuna helazakuhonga malefa tunahela zakusajili

    ReplyDelete
  8. Hivi jkt ruvu inazopesa za kuwahonga waamuzi kuliko Sumba? Au mohamed ndio kusema kafulia kaishiwa pesa za kununulia meche kama Mwaka Jana hahaha wape salamu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hela za Mo sio za mikia! Yeye mwenyewe kasema simba hawana hela...hehe

      Delete
  9. Mechi ya simba na yanga ilishaisha hawa waandishi walishaandika mengi mpaka sasa wanarudia rudia hakuna faida kuendelea kujadili,zungumzieni timu ya taifa acheni usimba na uyanga,au wenzetu mnafurahia sare?

    ReplyDelete
  10. Replies
    1. HEEH HEEH HEEH!!!!!!......KUANZIA SASA KILA MTU ASHINDE MECHI ZAKE HALAFU ILE YA MWISHO KATI YA YANGA NA MKIA,TUWAACHIE MIKIA WASHINDE PIA TUONE NANI ATAKUKUWA BINGWA.....HAAAH HAAH HAAH.....NACHEKA KWA DHARAAAAUUH!!!!!!!

      Delete
    2. Akili yako Ni utopolo mtupu, unamuwaza mumeo tu kila wakati na unamsahau anaeongoza ligi kwa sasa.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic