November 12, 2020


 KOCHA wa timu ya Taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps, amesema kiungo wa Manchester United, Paul Pogba, hana furaha na nafasi anayochezeshwa kwenye timu hiyo na kumfanya ashindwe kuwika msimu huu.

 

Deschamps amemkingia kifua kiungo huyo, kuwa alikuwa majeruhi kwa muda mrefu hivyo anahitaji muda wa kucheza ili kurejesha makali yake aliyokuwa nayo hapo awali.


 United inaonekana kukosa uwiano pindi wanapocheza na Bruno Fernandez, hivyo kumfanya Pogba kuanzia kwenye benchi.

 

"Pogba hana furaha ndani ya United kutokana na nafasi ambayo anachezeshwa kutokuwa yake ila nina amini kwamba bado ana uwezo mkubwa na akiaminiwa ataonyesha yale aliyonayo na watafurahi wenyewe," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic