December 29, 2020


 KIPA namba moja wa Klabu ya Majimaji, Mputi Jafary amesema kuwa uwezo wa kiungo wa Simba, Said Ndemla ulichangia kwa timu hiyo kupoteza mchezo huo kufungwa mabao 5-0.


Jafary alikaa langoni ndani ya dakika 90 ambapo aliokoa shuti moja la Ndemla dakika ya 15 na kusababisha kona na pia dakika ya 3 alikutana na shuti la Ndemla ambalo liligonga mwamba kabla ya kukutana na guu la Gadiel Michael aliyezamisha mpira wavuni.

Jaffary amesema:"Mabao matano ni mengi na yanaumiza kwa kuwa hatukutaka kufungwa ila kushinda mchezo na kusonga hatua ya mbele.


"Ila nyota aliyesababisha yote  yatokee ni yule kiungo Said Ndemla alikuwa anacheza na mpira namna anavyotaka na kuisumbua timu muda wote aliokuwa ndani ya uwanja.


"Ukiachana na hilo pia sehemu ya viungo wa Simba hapo ndipo ambapo palituharibia utulivu pia viungo wao muda wote walikuwa wanamiliki na kutengeneza hatari," .


Simba Desemba 27 iliibuka na ushindi wa mabao 5-0 kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho na kusonga mbele.


Mabao Uwanja wa Mkapa yalifungwa na Gadiel Michael, Chris Mugalu,Ibrahim Ame, Meddie Kagere na Luis Miquissone. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic