December 22, 2020


BARAKA Majogoro,nyota anayekipiga ndani ya kikosi cha Mtibwa Sugar anatajwa kuingia kwenye rada za mabosi wa mitaa ya Kariakoo, Simba na Yanga ambao wanataka kuipata saini yake.


Kwa sasa ni wakati wa usajili wa dirisha dogo ambalo lilifunguliwa Desemba 16 na linatarajiwa kufungwa Januari 15,2021.

Kiungo huyo mkabaji ambaye ni mzawa amekuwa na uwezo mkubwa ndani ya uwanja jambo lilowavutia mabosi wa Klabu za Simba na Yanga.

Mbali na timu hizo pia JKT Tanzania wanatajwa kuwania saini ya nyota huyo wa zamani wa Klabu ya Polisi Tanzania inayonolewa na Malale Hamsini.

Majogoro amesema kuwa kwa sasa yeye ni mali ya Mtibwa Sugar hivyo bado hajajua ishu yake ya kusepa ndani ya kikosi hicho.

4 COMMENTS:

  1. Acheni kuwapotosha watu mbona hapo sijaona mahali palipoandikwa yanaga au Simba wameongea nae halafu si Jana tu mmeandika hii habari iweje leo mrudie tunashindwa kuelewa mnapokwama

    ReplyDelete
  2. kiwango chake bado kwa hizi timu yuko slow bado na hapandishi timu juu yaani yule dogo wa polisi rasta pale kati mzuri kuliko huyu

    ReplyDelete
  3. Wanajitungia habari then kesho utasikia viongozi wa timu wamekanusha

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic