NYOTA Simba, Bernard Morrison amesema kuwa wanaamini watapambana kufika mbali kimataifa ili kuwapa furaha mashabiki na kutimiza malengo ambayo wamejiwekea.
Simba imetinga hatua ya mtoano Kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuing'oa Plateau United Kwenye mechi za hatua ya awali.
Mchezo uliowapa nafasi ya kupeta mazima ulikuwa ni wa ugenini uliochezwa Novemba 29 ambapo Simba ilishinda bao 1-0 Uwanja wa New Jos lilipachikwa na Clatous Chama kwa pasi ya Luis Miquissone.
Mchezo wa pili uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Desemba 5,Simba ililazimisha sare ya bila kufungana na kufanya ishinde hatua inayofuata ambayo ni ya mtoano.
Morrison amesema:"Ninaona kwamba mashabiki wanafurahi kuona tunasonga mbele hata sisi pia tunafuraha, kikubwa ambacho tunakwenda kukifanya ni kuongeza juhudi kwa ajili ya mechi zetu zijazo.
"Malengo yetu ni kuona tunafika mbali na hili linawezekana ikiwa kila mmoja anatimiza wajibu wake na ndicho tunachokwenda kukifanya," amesema.
Mchezo ujao wa hatua ya mtoano kwa Simba ni dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe.
Ijapokuwa ni yanga kindaki lskini naitakia simba kila la kheri kwasabsbu inaimathili nyota kwa nchi yetu
ReplyDeleteTrue, ww ni shabiki unyejua mpira achana na utopolo wengine ndani ya klabu yenu qasiyojua mpira kushindwa kutofautisha m ashundano ya kimataifa na kitaifa
DeleteNasema hivi simba inatakiwa kucheza mpira WA Kasi,kushambulia ikiwa inacheza nyumbani,mfumo WA kutumia mshambuliaji mmoja mechi za nyumbani siungi mkono,Kuna baadhi ya wachezaji hasa WA ndani hawana nguvu Na Kasi ya mchezo,Dilunga,Mzamiru Na Mkunde sio wale waliotufika robo fainal,wamepungukiwa mbinu wanaigeria hawakuwa mechi fitness ndio maana walichoka Sana Na kudondoka hovyo.Waliathiriwa Na Covid 19.Ikiendelea kucheza hivi kisa ushindi WA ugenini itakula kwetu.Nilitegemea tungepata goli la mapema ndio tucheze kwa kuzuia.Hivi wale jamaa kwa babati mbaya wangepata goli dk ya 85 Na kuendelea pressure ingekuwaje?Kweli mbinu za Kocha mbovu hasa mechi za home
ReplyDelete