December 5, 2020


 KOCHA Msaidizi wa Simba, Seleman Matola amesema kuwa watapambana kwa hali na mali kupata matokeo kwenye mchezo wa leo dhidi ya Plateau United utakaochezwa Uwanja wa Mkapa.


Kwenye mchezo wa kwanza Simba ilishinda bao 1-0 dhidi ya Plateau United uliochezwa Uwanja wa New Jos na leo ina kibarua cha mchezo wa marudio dhidi ya wapinzani wake hao kutoka Nigeria.

Tayari Plateau United imeshatia timu ndani ya Bongo, jana Desemba 4 kwa ajili ya mchezo wa leo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Matola amesema kuwa wanatambua mchezo utakuwa mgumu lakini watapambana kupata matokeo ili waweze kufikia malengo ambayo wamejiwekea.


"Ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji ushindi ila nasi tupo tayari kwa mchezo wa leo kikubwa ni kuona kwamba tunapata matokeo chanya.


"Mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti nasi tunaamini kwamba hatutawaangusha hasa ukizingatia kwamba tutakuwa nyumbani," amesema.


Matola atakuwa kwenye bechi la ufundi akiwa chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck raia wa Ubelgiji ambaye ni kocha mkuu.

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic