December 21, 2020

 


SHECKY Mngazija, daktari wa Klabu ya Yanga amesema kuwa nyota wao Lamine Moro huwa hapigwi sindano za ganzi ili aweze kucheza kwa kuwa yupo fiti ila kitu ambacho humkuta ndani ya uwanja ni sehemu ya mchezo.

Nyota huyo ambaye amekuwa mhimili mkubwa ndani ya kikosi hicho amefunga jumla ya mabao manne na kutoa pasi moja ya bao.

 Kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara uliopita wakati wakishinda mabao 3-1 dhidi ya Dodoma Jiji, beki huyo alionekana kutokuwa fiti jambo ambalo lilizua mjadala kwamba anasumbuliwa na majeraha ila anachezeshwa akiwa amepigwa sindano.


Daktari huyo amesema:"Lamine yupo fiti na hana majeruhi ambayo yanamsumbua pia hachezeshwi akiwa amepigwa sindano kwa sababu kanuni haziruhusu suala hilo.

"Kinachotokea ndani ya uwanja ni sehemu ya mchezo kwa sababu kila mchezaji anapambana kusaka ushindi kwa ajili ya timu yake jambo ambalo linamfanya naye awe kazi akisaka ushindi," amesema.

8 COMMENTS:

  1. ITAFIKA SIKU MTAMUWEKA BENCHI HAPO NDIPO YATAKUWA YAMETIMIA,LAMINE YEYE SIO TABIBU NA WALA HAJUI HII DAWA ANAPEWA KWA JILI YA NINI, SHIDA ANAONEKANE ANACHEZA TU

    ReplyDelete
    Replies
    1. Punguzeni ufinyi wa fikra....hivi huyo Lamime yeye ni mtoto mdogo mpaka akubali kuchomwa sindano ambayo anafahamu kuwa ina madhara na haikubaliki!!!.Hao wachezaji wetu wa kibongo tu ni wachache sana wasiojitambua,wengi wao hawawezi kukubali pia na kukubali kufanyiwa kitu kama hicho,itakuwa mchezaji wa kimataifa kama Moro?!!.Ukitafuta wachezaji watatu wa kigeni wanaojitambua Lamine huwezi kumkosa.

      Delete
    2. unao uhakika kuwa lamne anachomwa sindano?

      Delete
  2. Mpira wetu nao kila siku habari zisizo na mashiko

    ReplyDelete
  3. Isije ikafika akawa anapigwa sindano za kuongeza nguvu, hilo ni kosa kubwa ktk michezo. Kama anaunwa asilazimishwe kucheza

    ReplyDelete
  4. Hawa waandishi wanatengeneza habar za uongo makusudi ili baadae waje watengeneze nyingine ya kukanusha.... Hawiwezekani kila mara habari itoke mara mbili yani kuelezea jambo fulani halafu baadae kulikanusha.... Kama sio hivyo basi mkubali kuwa hamko makini katika kutafuta habari za uhakika ila mnakurupukaga tu

    ReplyDelete
  5. Maandishi anaandika mambo ya kujiunga Anaacha mambo ya msingi mfano Morrison katukana watu mwandishi amekuwa bubu. kazi ya kufuatilia mambo ya yanga kila siku utaumia sana.Mmezoea kuleta migogoro pale yanga

    ReplyDelete
  6. Na bado, mtachokonoa Yanga mpaka macho yawatoke.
    Mwacheni apige kazi.haiwahusuuuu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic