DIRISHA la usajili la Ligi Kuu Bara linatarajiwa kufunguliwa Desemba 15 ambapo kwa sasa unaweza kusema kwamba bado siku sita kuweza kufikia siku ya dirisha hilo kufunguliwa.
Kuna umuhimu mkubwa kwa kila timu kuanza maandalizi mapema kwani
matokeo chanya uwanjani yanatengenezwa na maandalizi ya awali ambayo timu huwa
zinafanya.
Muda wa kufanya haya yote ni sasa kwa kuanza kujipanga ili
kuweza kufanya usajili makini kwa wakati huu wa kufanya maboresho ndani ya
timu.
Kwa timu zote bila kujali zinashiriki Ligi Kuu Bara ama Ligi
Daraja la kwanza ni muhimu kujipanga vema.
Wale ambao wamekuwa wakifanya usajili kwa matakwa yao ama kutumia
nafasi zao za uongozi si sawa kwani anayejua uhitaji wa wachezaji ni kocha
mwenyewe.
Itapendeza endapo viongozi watafuata ripoti ya kocha kwenye
kufanya usajili jambo liakaloepusha lawama na malalamiko kwa benchi la ufundi
kwani wao ndio wanahusika kwenye suala la kupanga timu.
Kwa kupitia yale mapungufu ambayo benchi la ufundi limeyaona
hapo ndipo kazi inabidi ifanyike na sio kusajili kwa kufuata mkumbo.
Kila mmoja amekuwa ana mamlaka hasa linapofika suala la usajili
kulingana na mapenzi ambayo anayo kwa mchezaji ama wengine ni wale ambao
wanaona kwamba watapata faida endapo watamsajili mchezaji fulani.
Sasa suala la kutazama faida huwa linakuwa kwa muda tu tofauti
na yule ambaye atasajili kwa kufuata mapendekezo ya mwalimu itasaidia kujenga
kikosi imara.
Ikumbukwe kuwa wakati timu ikiboronga anayepewa mzigo wa lawama
siku zote huwa ni mwalimu hivyo itakuwa vizuri endapo ripoti itafanya kazi
lawama zitakuwa haziepukiki kwake.
Kwa wakati huu timu nyingi zimeona namna ambavyo zilikuwa kwenye
kusaka pointi tatu ndani ya uwanja pamoja na matokeo ambayo wamekuwa
wakiyapata.
Jambo la kuzingatia kwa sasa ni wachezaji makini na wazuri ambao
watakuwa na nidhamu nje na ndani ya uwanja hii itasaidia kuwa na benchi makini
pamoja na timu imara.
Muda mzuri kwa Shirikiso la Mpira Tanzania (TFF) kuendelea kutoa
taarifa mapema na masuala yote yanayohusu usajili kwa wanachama wake kwa wakati
huu.
Ikumbukwe kwamba kuna timu ambazo zimepanda daraja msimu huu
ikiwa ni pamoja na Gwambina FC, Ihefu,Dodoma Jiji hizi nazo pia zina jukumu ya
kuangalia pale ambapo zimekuwa na mapungufu.
Suala la kukurupuka kwenye usajili kwa wakati huu litakuja kutoa
majibu baada ya ligi kumalizika kwa kuwa dirisha dogo siku zote hutumika
kufanya maboresho kidogo na sio kikosi kizima.
Kama wachezaji watatukuwa kwenye mazungumzo na timu ni muhimu
kuangalia sehemu ambayo wanakwenda pamoja na nafasi yake huko.
Wachezaji wanatambua kwamba wakati unaokuja ni muda wa mauzo
hilo lipo wazi lakini lazima wasisahau kwamba kazi yao ni mpira hivyo lazima
wacheze.
Wakati wa usajili pia ni muda wa kuonyesha kwamba thamani ya
mchezaji uwanjani ilikuaje na nanmna gani anaweza kuwa msaada kule anakokwenda
jambo la msingi ni kujitambua.
Ikitokea mchezaji akapata timu na akakubaliana kuwa mchezaji wa
hiyo timu anayokwenda basi lazima aendane na utaratibu ambao ataukuta maisha ya
mchezaji ambaye hatambui kazi yake ni magumu kwa wakati ujao.
Kila kitu kwenye soka kinawezekana na ipo wazi kwa muda huu
malipo ya wachezaji yawe wazi na wajitoe kwa moyo mmoja kufanya kazi na
kutafuta matokeo.
Benchi la ufundi litazame namna bora ya kufanya kuweza kusajili
wachezaji makini ambao watasajiliwa kupitia ripoti ambazo zimeandaliwa.
Nidhamu inapaswa ipewe kipaumbele na wachezaji wawe makini
kuelekea kwenye maisha yao mapya ambayo watakwenda kuanza ni muhimu kuzingatia
kwamba maisha yanakwenda kasi sana.
Jambo la msingi kwa viongozi na mabosi wa timu kuzingatia usajili
kwa kufuata ripoti na sio mapenzi ya timu ama kiongozi fulani.
Wawakilishi wa kimataifa Simba na Namungo wana jukumu pia la
kuweza kufanya maboresho kwenye vikosi vyao ili kuweza kufanya vizuri kwenye
hatua za mbele.
Tayari nina amini kwamba benchi la ufundi limeona mapungufu
ambayo yapo kwenye timu zao hivyo jukumu lao ni kwenye kuboresha vikosi.







0 COMMENTS:
Post a Comment