December 17, 2020



KOCHA Mkuu wa Klabu ya Tottenham, Jose Mourinho amesema kuwa ushindi ambao wameupata wapinzani wake Liverpool kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu England ni wa kutengenezwa jambo ambalo halimpi tabu.


Ikiwa Uwanja wa Anfield ilikubali kichapo cha mabao 2-1 mbele ya Liverpool na kuifanya Tottenham kupoteza mchezo wa pili ndani ya Ligi Kuu England.

Roberto Firmino kichwa  chake cha dakika ya 89 kilipeleka msiba mazima ndani ya Tottenham na lile bao la kwanza kwenye mchezo huo lilipachikwa na nyota Mohamed Salah dakika ya 26 huku la kufutia machozi kwa Tottenham lilifungwa na Son Heung-min dakika ya 33.


Ushindi huo unaifanya Liverpool ya Klopp kuwa nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 28 huku Tottenham ikiwa nafasi ya pili na pointi zake 25.


Mourinho amesema:"Ushindi waliopata ni kutokana na makosa ambayo tumeyafanya kwenye kumalizia nafasi kwa sababu tulipata nafasi nyingi tukashindwa kuzitumia.

"Hakuna namna ni ushindi wa kutengenezwa ndani ya uwanja, wao walikuwa na presha kubwa na walikuwa wanahitaji kuongoza ligi wamefanikiwa.

"Nimewambia Klopp kwamba ameshinda mbele ya timu kubwa ambayo ilistahili kushinda ndani ya Anfield, siwezi kubadili matokeo kwa sasa kwa kuwa yameshatokea," .


1 COMMENTS:

  1. Huo haujatengenezwa wa kutengenezwa n wa mbeleko au mikia fc

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic