December 10, 2020



MSHAMBULIAJI wa Klabu ya Simba, Meddie Kagere ameungana na nahodha wake John Raphael Bocco kukanusha uvumi wa kuwepo ugomvi kati yao.

Kagere na Bocco walikuwa sehemu ya kikosi kilichoibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Polisi Tanzania jana Jumatano, huku tukio la kupishana kwa Bocco na Kagere wakati wa kushangilia bao la Chama likiibua Sintofahamu ya kutokuelewana kwa wawili hao.

Kagere kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram amesema: "Ningependa kuwa mkweli juu ya Suala hili linaonihusisha mimi na nahodha wangu John Bocco, kwa heshima kubwa niseme sijawahi kuwa na tatizo lolote na Bocco wala mchezaji yeyote wa Simba.

"Kwa upande wangu ni bora tukapambana na wapinzani wetu kuliko kupambana sisi wenyewe. Ni matumaini yangu kuwa mmenielewa na nawashukuru sana,".

Pia Bocco amesema kuwa anashangaa namna watu wanavyosema maneno ambayo hayana ukweli.

 


3 COMMENTS:

  1. Utopolo na waandishi wao.Utafikiri kuku anataka kutaga.
    Wanahangaika sana. Wanafanya kila mbinu kukutoa kwenye reli.
    Tuwapuuze wapuuzi hawa.

    ReplyDelete
  2. Mtaje t ni Maulidi Kitenge.ndo wanaemtumia kueneza huo upuuzi ni matukio mengi t ila mfikishien salam ipo ck tutamchoka atajuta anavyotumia.kuna ck alimuhoji muhuni fulan hiv wa yanga akisema mwanasheria ikawa wanazungumzia issue mabadiliko y Simba akaongopa mno mpka kiongoz mmoja wa Simba akapiga cm wasafi kuwaonya na kuwaambia wawe makini kazi yao hasa wanapotaka kutoa ufafanuzi wa jambo linalohusu sheria.kwaiyo Kitenge.anajitahd sana kuleta choko choko ndan y Simba at suala la Kagere.kupigana na kocha wakiwa mbeya kama ckusei ni yeye na aliliobgea mno moja Simba walipokanusha uyo ndo mwandishi adui mkubwa wa Simba kwasasa

    ReplyDelete
  3. Watu wanaitafutia simba migogoro ili wagombane wasifanye vizuli wachukukue wao kombe mmenoa pumbavu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic