December 11, 2020

 


IMEELEZWA Francis Kahata raia wa Kenya na mshambuliaji wa timu hiyo, Meddie Kagere raia wa Rwanda, hawana mpango wa kuendelea kuongeza mikataba ya kubaki ndani ya kikosi hicho huku kocha mkuu wa timu hiyo, Mbelgiji, Sven Vandenbroeck akitajwa kuwa chanzo cha wachezaji hao kuamua hivyo.

 

Kahata msimu uliopita alijiunga na Simba kwa mkataba wa miaka miwili ambapo huu ni msimu wake wa mwisho wakati Kagere alijiunga na Simba mwaka 2018 akitokea Gor Mahia ya Kenya kabla ya kuongeza mkataba unaofikia ukingoni mwishoni mwa msimu huu.

 

Taarifa kutoka ndani ya timu hiyo zinadai kuwa wachezaji hao hawana furaha kutokana na kocha huyo kushindwa kuwapa muda wa kucheza kadiri muda unavyokwenda licha ya kuwa wapo fiti hali inayopelekea wao kugomea kuongeza mikataba mipya iwapo kocha huyo ataendelea kuwepo.


Mtoa taarifa huyo alienda mbali kwa kusema kuwa hata kuondoka kwa Sharaf Eldin Shiboub raia wa Sudan kumechochewa na kocha huyo kushindwa kumpa nafasi ya kucheza.


 Kwa sasa vita hiyo imegeukia kwa mshambuliaji mzawa, Charles Ilanfya anayedaiwa kuomba kutolewa kwa mkopo katika dirisha dogo linalotarajiwa kufunguliwa Desemba 15, mwaka huu.

 

“Kahata na Kagere wao wameshasema hawataki kuendelea kubakia kucheza Simba kutokana na hali inavyokwenda kwa sababu mwalimu anaonekana kuwa tatizo kwao, hakuna ambaye yupo tayari hata ikiwa uongozi watahitaji wafanye hivyo.


 

"Hakuna anayeumwa kati yao isipokuwa mwalimu mwenyewe ndiyo hataki kuwatumia na hawajui kwa nini, hivyo kwa kuwa mikataba ipo ukingoni hawaoni haja tena ya kubakia.


"Kuondoka kwa Shiboub mwalimu wanadai amechangia lakini hata kwa sasa upande wa Ilanfya ambaye pia hamtaki licha ya kuwa alimsajili mwenyewe,” alisema mtoa taarifa kutoka ndani ya timu hiyo.



Chanzo:Championi

10 COMMENTS:

  1. WATULIE TU HAPO SIMBA, HELA SI WANALIPWA, HATA KAMA WANAKAA BENCHI MSHAHARA SI UNAINGIA? NA VIWANGO VIKISHUKA WATAACHWA WAKATAFUTE RIZIKI SEHEMU NYINGINE.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wachezaji wa kugeni ni tofauti na wazawa

      Delete
    2. Kipaji ndio kilicholeta mshahara, bila kipaji hakuna mshahara kwa hiyo cha kutunza kwanza ni kipaji sio mshahara kama kichwa nazi wa kwanza alivyoandika

      Delete
    3. Lazima utunze kipaji maana kikipotea pesa hautaiona tena. Ukizingatia na mpira na ndoto zina umri. Biashara mapema giza likiingia tinafunga mahesabu.

      Delete
  2. HAKUNA CHA KUSHANGAA HATA GUARDIOLA ALIMKATAA YAYA TOURE....KOEMAN HAMTAKI RQUI PUIG

    ReplyDelete
  3. Ushuzi mtupu ni jana tu mlishazua kuwa Boko na kagere wamepigana.Leo hii mnakuja na uzushi mwengine usio na mshiko. Kagere au kahata hawafanyi kazi simba bure wanalipwa tena vizuri tu wakiondoka sio simba itakayokosa kazi ni wao, na simba ni kubwa kuliko mchezaji yeyote yule.Takwimu na rekodi ya Sven tangu atue simba hakuna kocha Tanzania aliekuwa hata karibu yake kwa kipindi hiki tangu afike hapa.Tumeona timu kadhaa kdhaa zikifukuza na kubadilisha makocha kama kubadilisha nguo lakini simba wamekaa kocha wao ila hawapewi credit kwa hilo badala yake watu wanazua ya uongo ili kuipaka matope simba sisi watanzania mbona wa hovyo hivo,Simba ilikuwa ni timu iliyokosa nidhamu ndani na nje ya uwanja sven amerekibisha hilo.Simba waliwasajili kahata na Shibob kwa gharama kubwa kwa matumaini mkubwa yakuwa kaliba ya chama au kupita yeye lakini wakaja kuonesha viwango vya kawaida sana.Simba inahitaji wachezaji wa viwango kwa vitendo sio majina tu.Utamuekaje benchi Luis Miquisone umchesheze kahata? Kuna wachezaji au fowadi wenye uwezo zaidi ya kagere sema tu viongosi wa simba kama vile wamerogwa kwenye skauti ya wachezaji.Kuna tabia moja ya kijinga kabisa ya mashabiki wa simba inaendelea hivi sasa kujifanya wanajua kuliko benchi la ufundi la simba yaani hovyo kabisa.Sven ni kocha wa wa mataji na anaelewa utofauti wa mahitaji ya mechi mbali mbali na wachezaji husika. Mfano sven amaeleza mwezi wa kumi na mbili yaani December timu itacheza mechi kila baada ya siku tatu kwa hivyo ni vizuri kumpa nafasi kila mchezaji ili kubalance ratiba na kuwapa uzoefu wachezaji wengine.Mechi ya polisi Tanzania, simba ilishinda bao mbili kipindi cha pili kwa mabao ya chama ila bado mashabiki wa simba wakionekana kulalama kwanini akina chama wameanzia benchi? Wanashindwa kufahamu kuwa uwepo wa chama kwenye benchi kipindi chama kwanza ndio uliompa nafasi ya kusoma madhaifu ya polisi na kwenda kumaliza kazi kirahisi.Kagere hakuna anaebisha ni fowadi mzuri lakini anaendelea kuimarika taratibu baada ya injury.Lakini kama mashabiki wa simba wangekuwa weledi zaidi basi wangeandamana kushinikiza kocha kumpa namba ya kudumu Ibrahimu Ame kwenye eno la ulinzi ni beki hasa anepaswa kukomazwa kwani simba kumpoteza Ame ni hasara kuliko babu kagere.Mchezaji mwengine mashabiki wa simba kama wangekuwa wanaona kitaalamu zaidi basi wangeshinikiza kocha ampe namba kila ikiwezekana Said ndemla kwani kazi ya chama kwenye mechi ya polisi na simba ilikuwa rahisi kutokana na uwepo wa ndemla katikati ya uwanja.Ndemla amebadilika sana anagombania mipira na wachezaji wa timu pinzani kama mbwa na iwe mbwa na kuigawa kwa usahihi kabisa.Ni mchezaji anaepaswa kujengewa kujiamini zaidi kuliko hao wachezaji na wapambe wao wanaoitishia nyau simba.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nimekuelewa Sana ndugu has a baada ya kuwagusia Ame na Ndemla, madogo wanajua

      Delete
  4. Ninapoona coment Bora kma hii nafarijika mno we unaelewa tim inataka nn ila Kuna mashabiki wajinga tena sana wanafuatisha waandiahi wapuuzi mashabiki wa yanga wanaochokonoa mambo y kijinga kuona Simba inapotea ila hawataweza na ikibidi tukiona wanapitiliza tutawashushia kichapo wawe na adabu kiongozi wao ni Maulidi Kitenge.simba wampe nafasi Ame.pia Ndemla.wapo vizuri kuliko uyo Kahata.mshahara wa kahata na Ndemla.naamin kahata anakula pande kubwa zaid aondoke tena aondoke t waje wengine hana jipya pale Simba huo ndo ukweli

    ReplyDelete
  5. Naona baada ya kuisha la kagere na bocco ukaona uhamie kwa kahata tena mbn mnataman cmba ktokee migogoro hvo?????

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic