UONGOZI wa yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara jijini Arusha baada ya kudai kubaini hujuma wanayofanyiwa Dar.
Habari za kutoka ndani ya Yanga zinasema wamekuwa wakishinda kwa tabu kunatokana na njama chafu zinazofanywa na wapinzani wao, zinazosababisha wachezaji kuchoka kabla ya dakika 90 kumalizika.
“Tunadhani kuna mtu yupo ndani yetu anatumiwa, tena inawezekana tupo naye kila siku na anajipenyeza hadi kambini Kigamboni." kilisema chanzo chetu.
Alipotafutwa Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrik Mwakalebela ili aweze kuzungumzia juu ya suala hilo la timu ya Yanga kuwa kwenye mpango wa kuhama Dar aliweka wazi kuwa hakuna mpango huo.
"Kuhusu kuhama Dar na kuelekea Arusha kwa sasa hapana, hakuna mpango huo," .
Kazi imeanza!!!
ReplyDeletePumzi imekata. Visingizio vimeanza.Hata muhamie Burundi haisaidii.
ReplyDeleteHamna team bwana
ReplyDeleteNgoja mme wenu amalize na plateu and awachokonoe hko juu acheni kuweweseka
ReplyDeleteHakuna timu hapo mfukuzeni senzo huyo
ReplyDeleteSenzo anacheza namba ngapi?
DeleteNi hapo mwizi anapoogopa kuibiwa
ReplyDeleteUtopolo hali tete, na bado sana. Mtahamia Mtwara.
ReplyDeleteanayeandika habari hii ndiye chanzo
ReplyDeleteWote ni zero! Chanzo cha habari wapi?
ReplyDeleteWachezaji pumzi inakata mapema kipindi cha pili fanyieni kazi hili badala ya kutafuta sababu za nje ya mchezo hazisaidii saaana
ReplyDeleteTulieni na kila mtavobabaika ndipo mtavozidi kuanguka. Msiwasikilize waganga na nyie ndio mnaoutaka ubingwa. Watakumalizeni
ReplyDeleteKwani huko Arusha ndio Kuna nini na hiyo Ruvu Shooting watakubali kuburuzwa huko Arusha? Tulieni na mumtimuwe haraka huyo mbaya wenu nasi tumjue
ReplyDeleteMbona hata mikoani mnashinda kwa taabu? Kama anayewahujumu yupo karibu yenu, hata huko Arusha mtakuwa naye.
ReplyDeleteMechi za mikoani wanshinda kwa ushindi wa namna ganij
ReplyDeleteShari huzaa Shari na chakula chake ni shari
ReplyDeleteHongera Yanga. Baada kuifanyia hujuma Simba na wao kubaini na kuziba mianya ya hujuma kwa kuwafukuza mawakala wake.sasa na nyinyi mmebaini kuwa inawezekana Simba inaweza kulipiza. Hongereni mmeshtuka mapema. Simba walichelewa mkawachezea katika michezo karibu mitatu
ReplyDeleteHii taarifa Yanga wamekanusha. Hawahami Dar kuigopa hujuma bali watacheza mechi zao mbili mikoani. Kanuni inaruhusu timu kuchagua uwanja wowote kwa mechi mbili ndio maana KMC walipeleka mechi yao na Yanga jijini Mwanza. Pia mwaka juzi African Lyon walipeleka Arusha mechi zao dhidi ya Yanga na Simba. Au kwakuwa Yanga ndio mnaandika na visababu vya uongo mbona hamkuhoji why KMC mechi kapeleka Mwanza?
ReplyDeleteHii blog 80% ya habari zake ni za kubumba
ReplyDeleteUtopolo chali ngoja muanze kugongwa kila mechi, maana hata nje ya dar goli ni hilohilo moja tu. Mtafukuzana muda cmrefu wanaume twaja.
ReplyDeleteHakuna lolote saleh anabangaiza habari za kuandika. Angalia huko chini alivoishia hakuna kitu. Yanga haiwezi kuhamishia mechi Arusha. Timu haijapoteza game yoyote kuna haja gani ya kusema hayo? Huyu ni mwandishi mbumbaji tu
ReplyDeleteWacha waendeeeee
ReplyDelete