December 13, 2020

 


NYOTA wa Yanga, Tuisila Kisindaatafanyiwa vipimo zaidi ili kujua ukubwa wa tatizo pamoja na kupewa matibabu bora yatakayomrejesha uwanja kuendelea na kazi.

 Kwenye mchezo wa janan, Desemba 12 Uwanja wa Kambarage wakati Yanga ikishinda mabao 5-0 Kisinda alipata majeraha ya goti la mguu wa kushoto na alishindwa kuamaliza dakika 90.

 Kwa sasa inasubiriwa ripoti kutoka kwa daktari ili kujua tatizo lilivyo ili apewe matibabu haraka yatakayomrejesha kwenye kazi yake ya kutimiza majukumu ndani ya Yanga inayonolewa na Cedric Kaze.


Kwenye mchezo wa jana, Kisinda alifunga bao moja kwa pasi ya Yacouba Sogne dakika ya 56 na kuifanya timu hiyo kusepa na pointi tatu jumla.

Kaze amesema kuwa baada ya ripoti watajua ni muda gani mchezaji huyo atakuwa nje ya uwanja kwa matibabu kwa kuwa ripoti bado haijatoka. 

6 COMMENTS:

  1. Kuumia ni sehem ya mchezo. Kuumia ni kipindi katika vipindi wanavyopitia wachezaji

    ReplyDelete
  2. Kipindi cha krismas kuelekea mwaka mpya ni kibaya kwa majeraha ya wachezaji, kama hutaki muulize Arsener Wenger na Arsenal yake. Ndipo wachezaji muhimu wapo nje kichwa kinauma

    ReplyDelete
  3. Kuna kipindi wachezaji was Simba walikumbana na kuwa majeruhi, wakawa wanasemwa eti no sababu ya uzee. Sasa vijana wa Yanga wanaumia, sijui sababu ni ile ile au itabadilika

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic