December 3, 2020

 


NYOTA wa kikosi cha Yanga kiungo Mapinduzi Balama muda wowote kuanzia sasa anaweza kupelekwa nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.


Balama alipata maumivu ya mguu wa kushoto msimu uliopita wakati timu yake ikiwa kwenye maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ndanda FC.


Kwa sasa ameendelea kupewa huduma ya matibabu huku akishuhudia wenzake wakiendelea kupambana kupata matokeo ndani ya uwanja.


Daktari wa Yanga, Shecky Mngazija amesema kuwa kiungo huyo atakwenda Afrika Kusini ili kufanyiwa uchunguzi zaidi baada ya kukosekana uwanjani kwa muda mrefu.


"Ni kweli Balama Mapinduzi anaelekea Afrika Kusini kwa ajili ya kufanyiwa zaidi vipimo vya afya yake ili kuendelea mchakato na maendeleo yake.


"Taarifa zake tutaendelea kuzitoa kwani kwa sasa bado hatujajua kwamba itamchukua muda gani huko," amesema.


Mapinduzi atakumbukwa kwa uwezo wake wa mashuti akiwa nje ya 18 ambapo aliibuka shujaa kwenye dabi dhidi ya Simba alipomtungua Aishi Manula na kufanya Simba isiamini ilichokiona kwani baada ya dakika 90 ngoma ilikuwa 2-2.

5 COMMENTS:

  1. Mshammsliza huyo na hilo jeraha lishakuwa sugu,miezi yote hiyo munamchua na liliment tu, dah kipaji kwishnei!

    ReplyDelete
  2. Hapo wanazuga tu.wamemwacha muda mrefu sana

    ReplyDelete
  3. Muda wote huo kwanini hakupelekwa huko?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Uso wa binadamu umeumbwa na haya. Yanga wametahayari kuona Prince Dube aliyeumia juzi juzi tu amepelekwa Afrika sasa na wao wakaona wajitoe ufahamu wampeleke Balama baada ya jeraha kuwa sugu.

      Delete
  4. Hivi Fraga alipelekwa South Africa kwa matibabu? Au udhaifu unaonekana kea Yanga tu?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic