December 3, 2020

 


BREAKING: SAID Ntibanzokiza mshambuliaji mpya ndani ya kikosi cha Yanga, amewasili leo Bongo Desemba 2 rasmi kujiunga na Yanga baada ya kusaini dili la miaka miwili.


Nyota huyo amepokelewa na uongozi wa Yanga ikiwa ni pamoja na wadhamini wake Kampuni ya GSM kupitia Injinia Hersi Said pamoja na Ofisa Uhamasishaji,  Antonio Nugaz.



Pia Ofisa Habari, Hassan Bumbuli naye alikuwepo kwenye mapokezi ya nyota huyo raia wa Burundi.

Nyota huyo ambaye ametua kwa ndege ya usiku akitokea Burundi amepokelewa na mashabiki wengi ambao walijitokeza mapema kuanzia saa 1:00 usiku Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage, Nyerere.

Akizungumza muda mfupi baada ya kutua, mshambuliaji huyo amesema kuwa amefurahi kupata mapokezi makubwa na atapambana kufanikisha malengo ya timu.

Nugaz amesema kuwa kwa uwezo ambao nyota huyo anao lile tatizo la kutofunga mabao mengi litakwishwa na watafanya makubwa. 

4 COMMENTS:

  1. Sarpong na wenzake walipokelewa kwa kishindo cha kutisha na leo wanachokifanya uwanjani mwulizeni Kaze na mashabiki wa Yanga. Ni suala la muda kwake Saido

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sema Mukoko na Kisinda wakapokelewa na uwezo wao tumeuona muulize Onyango atakuambia Kisinda ni nani pia uluza nani alipewa million moja ktk derby ya Yanga vs Simba ni Mukoko sasa unataka mini cha zaidi

      Delete
    2. Hujaona faida ya yale mapokezi angalia msimamo wa ligi uone timu iko ya ngapi? Tatizo wabongo tunapenda vitu visivyo na msingi chenga; kukaa juu ya mpira nk.

      Delete
    3. Utopolo mtupu!👆
      Hamna kitu uwanjani kiualisia wote magalasa wamekuja kuuza sura bongo.
      Mshambuliaji haonekani,beki,kiungo wote Ni kizungumkuti. Pole utopolo lkn najua yote haya sababu ni ukapuku mlionao. Tafuteni fedha au mkapigie manji mmkopeshe team, hao GSM hawana hela.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic