December 31, 2020


 KIUNGO Jonas Mkude  wa Simba anaomba poo kwa rekodi kwa Feisal Salum, nyota anayekipiga ndani ya Klabu ya Yanga.

Kwa msimu wa 2020/21 Yanga ikiwa imecheza jumla ya mechi 17, Fei ameanza kikosi cha kwanza mechi 15 na kukosekana kwenye mechi mbili huku Mkude ambaye timu yake imecheza jumla ya mechi 15 ameanza kikosi cha kwanza mechi 9.

Pia kwa upande wa nidhamu Fei ameonyeshwa kadi moja ya njano licha ya kucheza mechi nyingi akiwa amefunga bao moja kwa Mkude ambaye amecheza mechi chache zaidi ya Fei ameonyeshwa kadi mbili za njano kwenye rekodi zake na hajafunga bao wala kutoa pasi ya bao.

Pia Mkude amesimamishwa na Klabu ya Simba kwa kosa la utovu wa nidhamu ambapo anatarajiwa kupelekwa kwenye kamati ya nidhamu ili kujibu tuhuma ambazo zinamkabili kiungo huyo mzawa.

Mkude jumla ametumia dakika 814 uwanjani katika mechi 10 ambazo amecheza kwa msimu wa 2020/21 ndani ya Ligi Kuu Bara alimaliza dakika 90 kwenye mechi 9 na mechi moja alitumia dakika 4.

Fei amemaliza dakika zote 90 kwenye mechi 13 ambazo ni daki 1,170 na mbili hakumaliza dakika 90 na kumfanya atumie jumla dakika 1,284 ndani ya uwanja.

Hizi hapa za Mkude Simba:-Ihefu FC dk 90Mtibwa Sugar dk 90Gwambina dk 4Prisons dk 90Ruvu Shooting dk 90Mwadui dk 90Kagera Sugar dk 90Yanga dk 90 mchezo huu alionyeshwa kadi ya njano mojaMbeya City dk 90 na KMC dk 90 ambapo pia alionyeshwa kadi ya njano moja.

Fei Toto ilikuwa mbele ya Tanzania Prisons alitumia dk 90Mbeya City 60, Kagera Sugar 90, Mtibwa Sugar 90, Coastal Union 90,Polisi Tanzania 90, KMC 90.
Simba 90 na alionyeshwa kadi moja ya njano.

 Namungo 90, Azam FC 90, JKT Tanzania 54, Ruvu Shooting 90.Mwadui 90, Dodoma Jiji 90 na Ihefu 90 ambapo alipachika bao lake la kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21.

 

8 COMMENTS:

  1. Mmebakiza kusema kibwana shomari amfunika kapombe kwa mipira kurusha

    ReplyDelete
  2. Tatizo la makahaba was kiume mikia akili zap ni moja,mi kwangu mkude Ana mazuri na few Ana maZuri ,bt bt mkude imara Lkn maarifa anayapa vipindi ,Fei sort kiasi bt Ana vision,Lkn kea Wachezaji wazawa kwenye namba yao ukitaka Mchezaji sold Mkude anapakata Tatizo lake Simba wanajua ,kwangu ni Kama Zawadi Mauya Lkn amemzidi focus(uangalizi/ wakati mwingine determination unaweza sema ,ila watu wa media punguzeni utapeli kujifanya mnajua na mmekuwa sehemu ya kupotisha mpira au michezo yetu,Mimi nadhani kazi yenu ni kushauri na kutoa taarifa kwa usahihi mnayo yaona .Lakini pamekuwa na upotoshaji wa maadili mmekuwa Makocha,Viongozi ,Referees,mpaka mamlaka za maamuzi.Ila ukweli ninyi mmekuwa ma ripota wa Siasa ,Dini

    ReplyDelete
  3. Extremely inspired! Everything is extremely open and clear illumination of issues. It contains really certainties. Your site is extremely important. Much obliged for sharing. 안전놀이터

    ReplyDelete
  4. Positive site, where did u come up with the information on this posting?I have read a few of the articles on your website now, and I really like your style. Thanks a million and please keep up the effective work. 사설토토

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic