LAMINE Moro beki wa kati wa Yanga na nahodha wa kikosi hicho amehusika kwenye jumla ya mabao manne kati ya 22 ambayo yamefungwa na timu yake hiyo kwa msimu wa 2020/21.
Ikiwa imecheza mechi 15 kibindoni imejikusanyia pointi 37 inafuatiwa na watani zake wa jadi Simba wenye pointi 29 baada ya kucheza mechi 13.
Moro anashikilia rekodi ya kuwa kinara kwa mabeki wenye mabao mengi ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21 akiwa nayo matatu.
Mabeki wengine wenye mabao ni pamoja na Pascal Wawa na Joash Onyango wa Simba, David Luhende wa Kagera Sugar wote wametupia bao mojamoja.
Katika mchezo uliochezwa Desemba 12 dhidi ya Mwadui FC beki huyo mwili jumba aliweka rekodi yake kwa kuhusika Kwenye mabao mawili kati ya matano ambayo Yanga ilishinda.
Alitoa pasi moja ya bao na alifunga bao moja na kumfanya afikishe jua ya mabao matatu huku akiwa na pasi moja.
Jumla amehusika katika mabao manne kati ya 22 ndani ya timu hiyo ambayo haijapoteza mchezo mpaka sasa kati ya 15 iliyocheza ndani ya Ligi Kuu Bara.
Mwandishi twajua kafunga mabao 4 ,nawe ukakiri mabao 4 then unaandika 3 ,labda human error
ReplyDelete