December 14, 2020

 


JOHN Bocco, nahodha wa Simba ndani ya misimu miwili mfululizo ameiadhibu Mbeya City na kuipa timu  yake pointi tatu muhimu. 


Msimu wa 2019/20 wakati Simba ikishinda mabao 2-0 Uwanja wa Sokoine na kusepa na pointi tatu, Bocco alitupia mabao yote mawili.


Msimu huu pia wa 2020/21 wakati Simba ikishinda bao 1-0, Bocco alitupia bao la ushindi na kujenga ushkaji na Uwanja wa Sokoine kila wakutanapo na Mbeya City. 


Ndani ya misimu miwili, Bocco amewaadhibu Mbeya City nyumbani kwa juma ya mabao matatu ambayo yamefanya Simba ikusanye jumla ya pointi sita.


Ushindi wa jana, Desemba 13 unaifanya Simba kufikisha pointi 29 na kuishusha Azam FC nafasi ya pili kwa kuwa ina pointi 27 na imecheza mechi 14 leo ina kazi mbele ya Namungo FC.

1 COMMENTS:

  1. Kwakweli mimi ni miongoni mwa watu wanomsema John Boko mara nyingi tu kwa kushindwa kujitambua ila kwa goli alilofunga Jana zidi ya mbeya city John Boko ameonesha kuwa anaweza na hapo ndipo wadau wanaomponda Boko ugomvi unapoanzia kwani Boko uwezo anao mkubwa ila wakati mwengine mtu unawaza John Boko anasumbuliwa na nini? Ni mtu mwenye papara na kukosa umakini katika umaliziaji wakati mwengine bila sababu na ndio maana watu huwa hawaachi kumtajataja kagere ila nnaimani Boko ameimarika sasa. Akitulia tu kwenye eneo la umaliziaji basi hakuna fowadi wa kumkamata John Boko kwenye Ligi, yupo vizuri aongeze bidii tu kwani Christian Ronaldo na ubora wake lakini gym ni sehemu ya maisha yake ya kila kitu kuhakikisha kuwa anaufanisi bora unaohotajika katika kazi yake.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic