December 8, 2020


NYOTA mpya wa Klabu ya Simba ambaye ni kiungo mkabaji, Taddeo Lwanga amesema kuwa amekiona kikosi chake kipya kikiwa kazini jambo linalomfanya aongeze nguvu mazoezini ili kupata namba kikosi cha kwanza.


Wakati Simba ikitoshana nguvu ya bila kufungana na Plateau United kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Desemba 5 Uwanja wa Mkapa alikuwa akishuhudia mchezo mzima kwa kuwa tayari yupo zake ndani ya ardhi ya Tanzania.

Jana Desemba 7 kiungo huyo ambaye amepewa majukumu ya Gerson Fraga alianza mazoezi na kikosi chake kipya ambacho kinajiandaa na mchezo wa ligi kuu bara dhidi ya Polisi Tanzania utakaochezwa kesho, Desemba 9, Uwanja wa Mkapa.

Lwanga amesema:"Nimekiona kikosi kwenye mchezo wetu dhidi ya Plateau United, kuna wachezaji wengi wazuri na wenye uzoefu hivyo nina amini kwamba nina kazi ya kufanya ili kuwa bora.


"Kwa namna maisha hapa yalivyo ninafurahi kuwa hapa ninaamini kwamba tutashirikiana na wenzangu ili kupata kile ambacho tunakihitaji," .


Mchezaji huyu ni wa kwanza kusajiliwa na Simba ikiwa ni kuelekea kwenye maadalizi ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya mtoano, amesaini dili la miaka miwili.

 

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic