Kocha huyo mwenye mbwembwe nyingi na maneno kibao, Jumapili ya Desemba 6, Uwanja wa Tottenham aliingoza timu yake kushinda mabao 2-0 dhidi ya Arsenal kwenye mchezo wa Ligi Kuu England ambapo umiliki wa mpira kwa timu yake ilikuwa ni 30 huku Arsenal wakiwa na 70.
Mourinho alishuhudia mabao hayo yakifungwa na Son Heung-min dakika ya 13 na nahodha Harry Kane dakika ya 45+1 na kuifanya timu yake kukaa kileleni ikiwa na pointi 24 baada ya kucheza mechi 11 huku Arsenal ikiwa nafasi ya 15 na pointi 13.
Pia nahodha Kane amesema kuwa timu inafurahi kucheza katika mfumo wowote lengo lao ni kuona wanapata matokeo ndani ya uwanja jambo ambalo linawafanya wacheze bila presha ndani ya dakika 90 huku wakifanya mashambulizi ya kushtukiza.
Mourinho amesema :"Unapozungumzia habari za umiliki wa mpira hiyo ni falsafa ya kwenye mpira lakini kwangu mimi naona matokeo ni muhimu zaidi, hakuna hata mmoja ambaye amewahi kuona nimepoteza mchezo ila nimekuwa na umiliki mkubwa wa mpira.
"Jambo la msingi ni kile ambacho unakifanya na mpira ndani ya uwanja hakuna jambo lingine zaidi ya ushindi, wachezaji wangu wanapenda na wanafurahi.
"Nakumbuka wakati watu wanasema kwamba uwezo wangu umekwisha ila niliweza kutwaa mataji matatu ndani ya Manchester United, nilishinda Super Cup na Europa League sasa wananiambia nimechuja hebu fikiria wapo wengine hawana kabisa haya mataji sasa sijui itakuaje," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment