December 12, 2020



IMEELEZWA kuwa nyota wa zamani wa kikosi cha Yanga ambaye kwa sasa maisha yake ya soka yapo zake ndani ya Kagera Sugar,  David Luhende jina lake linapigiwa hesabu na mabosi wake wazamani ili wamrejeshe kundini.


Luhende amekuwa bora ndani ya Kagera Sugar chini ya Mecky Maxime akiwa ni beki kisiki chaguo namba moja ndani ya timu hiyo.


Msimu uliopita wa 2019/20 jina lake lilikuwa ndani ya tatu bora ya mabeki bora wa Ligi Kuu Bara aliweka rekodi ya kucheza jumla ya mechi 38 akiyeyusha dakika zote 90 na kumfanya atumie jumla ya dakika 3,420.


Msimu huu wa 2020/21 ameyeyusha dakika zote 90 kwenye mechi 14 na kumfanya atumie jumps dakika 1,260 akihusika Kwenye mabao manne kati ya 12, ametoa pasi tatu na kufunga bao moja.


Cedric Kaze,  Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa kuhusu usajili ni mpaka pale atakapomaliza mzunguko wa kwanza atajua nini anahitaji.

4 COMMENTS:

  1. Ana umri gani? Maana mlisema hamsajili wazee..... Mtasajili Sana Ila ubingwa msahau

    ReplyDelete
  2. Pumbavu kabisa,kwa uwezo gani alionao?alipata bahati ya kucheza Yanga kipindi kile timu ikiwa haina uwezo wa kusajili lakini si kwa kuwa na kiwango bora cha uchezaji

    ReplyDelete
  3. Utatazitapika hizo pesa unazopewa kupigia Promo wachezaji.

    ReplyDelete
  4. Wanaoamini kila liandikwalo na mtandao huu mtakuwa na matatizo ya akili

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic