December 12, 2020

 


BAADA ya kikosi cha Polisi Tanzania kupoteza mchezo wake uliopita Desemba 9 Uwanja wa Mkapa kwa kufungwa mabao 2-0 mbele ya Simba, leo inakutana na wajeda Ruvu Shooting Uwanja wa Ushirika,Moshi.


Kikosi kilisepa Dar,Desemba 10 ili kuanza maandalizi ya mchezo wa leo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa ni vita za mbinu za makocha wazawa.


Malale Hamsini wa Polisi Tanzania anakutana na Charles Mkwasa wa Ruvu Shooting ambaye mkononi ana tuzo ya kocha bora ndani ya Ligi Kuu Bara ndani ya Novemba. 


Ikumbukwe kwamba Ruvu Shooting iliinyoosha Simba Uwanja wa Uhuru bao 1-0 na kusepa na pointi tatu muhimu kwenye mchezo huo ambao nyota wa Simba John Bocco aligongesha kwenye mwamba penalti.


Ofisa Habari wa Polisi Tanzania,  Frank Lukwaro amesema kuwa wanaweka kando matokeo yote mabovu wanaanza upya kusaka heshima.


Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema hawataki utani siku zote wanaingia uwanjani wakihitaji pointi tatu muhimu.


Hivyo leo Uwanja wa Ushirika Moshi ni vita ya wajeda walipokutana na Simba ndani ya Uwanja 

4 COMMENTS:

  1. Kiukweli hii ni habari ya kiwango cha chini mno, haieleweki. Waandishi mnafeli wapi? Kwani ni lazima kila stori uihusishe na simba hata pale haina uhusiano? Lengo ni nini hasa, kuipandisha hadhi?

    ReplyDelete
  2. Hii hutokea pape wanapokuwa hawana cha kuandika

    ReplyDelete
  3. Halafu mara nyingi wanatafuta habari hasi za simba kule yanga wanacheza na mwadui lakini habari ni simba tu wanasahau mwadui waliharibu rekodi ya yanga chini ya zahera ngoja siku serikali igeukie waandishi kanjanja wa michezo vilaza watakuwa wengi sana

    ReplyDelete
  4. Hizo timu zote mbili zimeshacheza na yanga mbona husemi unasema Simba tu. Halafu inaonesha waandishi wengi hawana uelewa mzuri wa michezo ndo maana wanajiandikia hovyo hovyo tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic