December 28, 2020

 


BAO pekee la Ismael Mhesa nyota wa Mtibwa Sugar dakika ya 47 linaipa nafasi timu hiyo kusonga mbele hatua ya nne ya Kombe la Shirikisho.

Mtibwa Sugar ilishinda bao 1-0 dhidi ya Geita Gold inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Ushindi huo unaifanya timu hiyo kuifungashia virago jumlajumla Geita Gold kwenye hatua ya tatu iliyokuwa na ushindani mkubwa. 

Mchezo huo wa Kombe la Azam Sports Federation Cup ulipigwa Desemba 27.

Bingwa wa taji hilo anapata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo kwa sasa taji hilo lipo mikononi mwa Simba inayonolewa na Sven Vandenbroeck.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic