UONGOZI wa Mtibwa Sugar umeweka wazi kwamba upo tayari kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC unaotarajiwa kuchezwa Desemba 11, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Mtibwa Sugar chini ya kocha msaidizi, Vincent Barnaba itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Ikiwa nafasi ya 13 na pointi 16 baada ya kucheza mechi 14 inakutana na KMC iliyo nafasi ya tano na pointi 21 baada ya kucheza michezo 12.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa kikosi kipo tayari na wachezaji wapo na ari kubwa ya kusaka ushindi.
"Wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya KMC, tunajua kwamba utakuwa mchezo mgumu lakini hakuna namna tupo tayari kwa ajili ya mchezo huo.
"Mashabiki watupe sapoti waone namna timu yetu inavyotoa soka makini na la kuburudisha ndani ya uwanja hatutawaangusha," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment