December 22, 2020

IMEELEZWA kuwa nyota wa Klabu ya FC Lupopo inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Congo yupo kwenye rada za kuibukia ndani ya Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina.

Mwamba huyo anatajwa kuingia kwenye reda za mabosi wa Azam FC ambao wanahitaji kuipata saini yake kuongeza makali kwenye safu ya ushambuliaji.

Awali jina lake lilikuwa linatajwa kuingia anga za Yanga inayonolewa na Cedric Kaze baada ya mabosi wa Jangwani kuipata saini ya Saido Ntibanzokiza wameweka kando dili hilo. 

Nyota huyo atapewa mikoba ya Thiery Akono Akono ambaye ameibukia nchini Malysia akitokea Klabu ya Azam FC ambayo alijiunga nayo msimu huu wa 2020/21.

Ofisa Habari wa Azam FC hivi karibuni aliweka wazi kuwa mpango wa kusajili upo na utawekwa wazi kwa kuwa dirisha la usajili bado halijafungwa.

6 COMMENTS:

  1. Hii ya Kila nyota kusajiliwa Simba au Azam kuonekana alitakiwa na Yanga b4 nayoo inahitaji kufikilika.Ali Niyonzima,Bwalya,Ame,Awesu,Ilanfya,no na wote tunaambiwa wame flop

    ReplyDelete
  2. Mchezaji mzuri hajifichi.. hata anaposhindwa kuperfom kwenye timu anayokwenda ni matokeo ya mpira tu.

    ReplyDelete
  3. Mtaendelea kuingia chaka kwa ajili ya kutaka kuikwamisha Yanga kwa manufaa ya Simba. Mlimchukua Domayo; Kavumbagu;Ngoma;Chirwa lengo kuihujumu Yanga. Sasa mkisikia mchezaji kaandikwa anatakiwa na Yanga mnamkatizia juu kwa juu. Hamuiwezi Yanga nyie mnajisumbua tu. Ali Niyonzima anawasaidia mini?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tafuteni pesa acheni mawazo yakiutopolo a.k.a ukiazi, Kama huna hela hata mke utapokonywa. Mwanaume halalamiki kwakuongeza sana kwamaneno mengiii bali huangalia tatizo chanzo chake na kutafutia ufumbuzi. Tafuteni pesa wacha maneno mengi.

      Delete
  4. Wacha ujinga wako wewe.Kwani Azam gana hski ya kusajili?
    Umekuwa stuffed up na Yanga hata huoni kwamba kuna timu zingine. Ukipofu fungua macho.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic