December 11, 2020


 IKIWA ipo nafasi ya kwanza na pointi 34 baada ya kucheza mechi 14 inaelezwa kuwa nyota sita ndani ya Yanga watapigwa chini kwa msimu wa 2020/21 kutokana na kushindwa kufiti kikosi cha kwanza.


Chini ya Kocha Mkuu, Cedric Kaze nyota hao wamekuwa wakikosa namba kikosi cha kwanza kutokana na sababu mbalimbali ambapo kocha huyo aliweka wazi kwamba wale ambao wanakaa benchi bado uwezo wao haujawa bora.


Imekuwa imara kwenye safu ya ulinzi inayoundwa na mzawa Bakari Mwamnyeto na Lamine Moro ikiwa imefungwa mabao matano kwenye mechi hizo 14.


Kesho, Jumamosi, Desemba 12 Yanga itashuka Uwanja wa Kambarage kusaka pointi tatu mbele ya Mwadui FC ambayo mwendo wake ni wa kusuasua kwa msimu wa 2020/21 ikiwa nafasi ya 17 na pointi 10.


Habari zimeeleza kuwa nyota hao ambao watatolewa kwa mkopo ni Juma Mahadhi, Adeyum Saleh, Wazir Junior, Paul Godfery, Said Makapu na Abdalah Shaibu,'Ninja'.


"Kuna ripoti ambayo imeshaandaliwa na imewataja kabisa nyota hao ambao watatolewa kwa mkopo ili kupata changamoto mpya, hivyo ni suala la muda tu kutimia," ilieleza taarifa hiyo.


Kwa upande wa Kaze kuhusu masuala ya usajili ameweka wazi kuwa kwa sasa hesabu zake ni kwenye pointi tatu kwanza ndipo atafikiria kuhusu masuala hayo. 

3 COMMENTS:

  1. ACHA KUPOTOSHA KAMA UNATUMIWA WAAMBIE WALIOKUTUMA WAACHE HABARI ZA KUPOTOSHA

    ReplyDelete
  2. Kila siku unakuja na list mpya Leo Makame umemsahau? Ndio ubaya wa habari za kuota usingizini.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic