December 12, 2020


KESHO Simba itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu muhimu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City utakaochezwa Uwanja wa Sokoine.


Wachezaji saba watakosekana kwenye kikosi hicho kutokana na sababu mbalimbali ambazo zimewafanya waweze kubaki Dar na wengine wapo nje ya Dar.

Thaddeo Lwanga kiungo mkabaji ndani ya Simba ikiwa ni ingizo jipya akiwa ni mchezaji huru licha ya kuanza mazoezi na timu bado hajapata nafasi ya kuwa kikosi cha kwanza mpaka pale usajili wake utakapokamilika dirisha dogo litakapofunguliwa Desemba 15.

Ibrahim Ajibu kiungo mshambuliaji, Charles Ilanfya mshambuliaji wa timu hiyo,Kennedy Juma beki wa kati na kiungo Bernard Morrison hawakusafiri na timu jana Desemba 11 kuelekea Mbeya.


Pia nyota Larry Bwalya raia wa Zambia huyu ana matatizo ya kifamilia akiwa zake nchini Zambia na anatarajiwa kurudi muda wowote na David Kameta beki wa kulia ambaye yupo na timu ya taifa ya chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes ambayo imeweka kambi Saudi Arabia.

3 COMMENTS:

  1. Hakuna upungufu wowote katika line up ya kawaida ya Simba maana hao wote huwa hawaanzi katika kikosi cha kwanza na hata Morrison huanzia benchi kisha huingia kama sub.Usipotoshe uhalisia

    ReplyDelete
    Replies
    1. Vipi Morrison,si yupo kwenye kiwango cha juu Sana kwa Sasa?

      Delete
    2. Yes,kiwango chake kipo juu zaidi ya hapo awali na ndo maana kocha humtumia katika kutafuta au kubadilisha matokeo kulingana na mchezo.
      Una swali jingine?

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic