December 14, 2020

 


KIUNGO mzawa ndani ya kikosi cha Yanga,  Feisal Salum wengi wanapenda kumuita Fei Toto ameingia Kwenye anga za Klabu ya TP Mazembe ya Congo.


Mbali na Toto pia beki mzawa wa kati  Bakari Mwamnyeto anatajwa kuingia kwenye rada za vigogo hao wa soka ndani ya Afrika. 


Wazawa hawa wote wawili wana nafasi ya kucheza timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na kwenye mchezo uliopita wa kufuzu Afcon dhidi ya Tunisia Uwanja wa Mkapa walikuwa na kikosi.


Fei Toto alifunga bao lililoipa pointi moja Stars kwenye sare ya kufungana bao 1-1 huku Mwamnyeto akipambana na Watunisia hao kwa dakika 90.

Ikiwa dili lao litajibu ndani ya Yanga kuna uwezekano wa nyota hawa wawili kusepa ndani ya Yanga ili wakapate changamoto mpya nje ya Bongo.

Ofisa Habari wa Yanga,  Hassan Bumbuli amesema kuwa kwa sasa bado wanajadili juu ya ofa ambazo zimewafikia mezani ili waweze kutoa taarifa kwa mashabiki.

11 COMMENTS:

  1. Si waende tu kila siku blah blah.kwanini hawafanyi kama wenzao simba ukisikia mchezaji wa simba anakwenda timu fulani iwe ndani au nje huwa sio propaganda ball huwa ni kweli.

    ReplyDelete
  2. Hii ni habari ya muda mrefu sana na mwandishi baada ya kukosa kitu cha kuandika unaamua kuirudisha. Kama hamna habar mpya tafadhali achen upuuz wa kurudia habar bila sababu za kuelewek

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hivi hamuwezi kuacha kuingia humu ?
      Kila siku kulalamika kama Mjamzito, then Baadaye utaingia tena..... Stupidity.

      Delete
  3. Kwa yanga hao wataozea hapahapa

    ReplyDelete
  4. Utopolo limbukeni hawajui mpira biashara, ukitaka kutoka kimataifa toka utopolo hamia kwa wajanja la sivyo utaozea vpl na mapinduzi cup

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nyie ndio maana Rage aliwaita mbumbumbu, mnaamini kila kilichoandikwa kwenye mtandao ni kweli! Mbona hamjamuuza MK 14 kwenda Spain? Tumieni akili kidogo alizowapa Mwenyezi Mungu

      Delete
  5. Utopolo wamejaa wivu viongozi wao na mpaka wanawaambukiza na baadhi ya mashabiki wao kuzuia ridhiki ya wachezaji wao nje na kudumaza soka la nchi. Ndo maana wachezaji wenye uelewa wakufika mbali hukimbilia Simba au Azam ha Kuna wivu huku. Ofa ikija mezani unapelekwa nje ukapate maisha Bora na kukuza kiwango chako zaidi
    *Utopolo badilikeni mpira biashara*

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani ninyi mmeshawaruhusu wangapi wakacheze huko nje safari hii? Wenye mtazamo huu akili zenu ni finyu sana na hamna uelewa wa masuala ya mchezo wa soka na mikataba. Kama jambo linaongelewa mitandaon tu na halijaenda klabuni unadhani nani anaweza kulifanyia kazi?

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic