STEPHEN Sey, mshambuliaji namba mbili ndani ya kikosi cha Namungo FC amesema kuwa leo watapambana kupata pointi tatu mbele ya wapinzani wao Azam FC.
Sey raia wa Ghana ametupia mabao mawili ndani ya Namungo FC inayonolewa na Hemed Morroco kati ya mabao nane ambayo yamefungwa na timu hiyo.
Kinara wa mabao ni Bigirimama Blaise mwenye mabao manne na mwingine mwenye mawili ni Lukas Kikoti.
Sey amesema:"Utakuwa mchezo mgumu ila tunahitaji pointi tatu muhimu kwa kuwa maandalizi yamekwenda vizuri nasi tumejipanga.
"Wapinzani wetu tunawaheshimu kwa kuwa ni timu imara na inafanya vizuri hilo lipo wazi ila tutapambana kupata matokeo.
Ikiwa nafasi ya 14 leo Namungo inakutana na Azam FC iliyo nafasi ya tatu baada ya jana kushushwa nafasi ya pili na Simba.
Azam FC ina pointi 27 kibindoni inakutana na Namungo FC Desemba 14 ndani ya Azam Complex ikiwa na pointi 16 ndani ya Ligi Kuu Bara.
0 COMMENTS:
Post a Comment